@jamiivoice_: HABARI: Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado, amesema mabadiliko ya makatibu wote wa mikoa wa CCM si jambo la kawaida, akidai kuwa yanaonyesha kuwepo kwa minyukano ya ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa ndani wa mwakani na Uchaguzi Mkuu wa 2030. Ado amesema hayo Oktoba 1, 2026 katika mikutano yake iliyofanyika Kata ya Mijelejele, Jimbo la Lulindi na Masasi Mjini, akidai kuwa minyukano hiyo inaratibiwa na kudhibitiwa na vyombo vya dola badala ya CCM yenyewe. Amedai kuwa CCM imepoteza udhibiti wa siasa za nchi na kwamba kwa sasa siasa zinaendeshwa na vyombo vya dola. Kwa mujibu wa Ado, mazingira ambayo vyombo vya dola vinaendesha siasa badala ya vyama vya siasa yanaweza kuathiri hali ya usalama nchini. Hata hivyo, Ado amesema yuko tayari kuendelea na kile alichokiita mapambano ya kisiasa licha ya vikwazo, akisema ukimya unaweza kuongeza kero kwa wananchi.
Jamii Voice
Region: TZ
Friday 02 October 2026 09:17:21 GMT
Music
Download
Comments
muhhamed :
ado sema sera acha kujaduli chama kingine
2026-10-02 09:58:32
3
Nassor cholo :
sasa nyinyi mbona munapenda kutufwatilia
CCM OYEEEEÈ
2026-10-02 15:18:49
1
Mariam Mugasha :
toa unafiki mabadiliko kwenye Chama Cha Mapinduzi ni kawaida
2026-10-02 12:19:57
1
mwile :
anaweka watuwake
2026-10-02 18:16:11
0
A>FATHER>FIGURE :
huyu nikimuendekeza atatupeleka mrama ila ninacho kihisia. akitoka ACT anahamia ccm
2026-10-02 09:30:31
0
mwile :
kwel kabisa kakangu edo
2026-10-02 18:17:49
0
Omar Suleiman :
sasa hayo yanawahusu nn
2026-10-02 14:18:53
0
Halima Funege :
huyu mbunge mm Toka nimeanza kuftiria siasa sijawahi kumuona akiongerea matatizo ya jimbu rake🤣🤣🤣🤣
2026-10-02 11:28:51
0
user9818422584475 :
WANAOKUTUKANA ACHANANAO HAO NIMISEKULE YA CCM WAVUNALANA
2026-10-03 06:22:28
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm
homepage.