@uhondo.tv: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amewasili katika Jiji la New Alamein nchini Misri, kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Nane wa Uratibu wa Katikati ya Mwaka wa Umoja wa Afrika (AU Mid-Year Coordination Summit). Mkutano huo unaofanyika kuanzia Oktoba 2, 2026, unafanyika chini ya kaulimbiu “Africa on the Land of El Alamein” na unawakutanisha viongozi wa ngazi za juu kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa na kikanda. Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Alamein, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Michezo na Vijana wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Gohar Nabil, Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo, pamoja na maafisa mbalimbali wa Serikali za Misri na Tanzania. Mara baada ya kuwasili, Mhe. Ndejembi amepokea taarifa kuhusu maandalizi ya Tanzania kushiriki katika mkutano huo, unaolenga kujadili na kuratibu masuala muhimu yanayohusu maendeleo na ushirikiano wa Bara la Afrika, ikiwemo uchumi, amani, usalama na ushirikiano miongoni mwa mataifa ya Afrika. Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unaendelea kuimarisha nafasi ya nchi katika Umoja wa Afrika na kutoa fursa ya kuchangia mijadala kuhusu utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo ya Bara la Afrika. #UhondoTVUPDATES

Uhondo TV
Uhondo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 03 October 2026 13:46:31 GMT
25314
692
8
23

Music

Download

Comments

tibuprime_
Mzee_wa_mifumo😎 :
Piga kazi vice president Ndejembi
2026-10-03 17:40:39
0
djamilah.kambangwa
djamilah kambangwa :
Mungu akutunze familiar
2026-10-03 18:34:51
0
user51800595670533
Abuubakary said njanga :
huyu nda kiongozi wa kitaifa .
2026-10-03 17:41:16
0
wilfredwilliam84
zinjatroupaz :
Safi sana
2026-10-03 15:51:20
0
user8551510439528
Hadahayo :
ila wagogo busara imetangulia mbele aise
2026-10-03 16:54:01
0
daniel.joseph938
Daniel joseph :
safi kabisa mula
2026-10-03 16:42:44
0
user131561855
user131561855 :
baba pigaa kazi yuda alikuwaa anatuvheleshaa
2026-10-03 16:23:10
0
dhimusha
Dhia muhammad :
Kidume huyoo 💛💛💛👍👍👍
2026-10-03 15:12:13
0
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About