@jambotv_: VIDEO: Serikali imetangaza kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha tathmini ili kuanza kulipa fidia ya awamu ya pili kwa wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani waliotwaliwa maeneo yao kupitia mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ). Hatua hiyo imebainishwa leo Jumamosi Oktoba 3, 2026 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kipaumbele katika eneo hilo. Akiwasilisha maombi ya wananchi waliosubiri fidia kwa muda mrefu, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Subira Khamisi Mgalu ameeleza kuwa ingawa baadhi ya maeneo tayari yamelipiwa fidia na mengine bado, matunda ya mradi huo tayari yanaonekana kupitia fursa za ajira kwa vijana wa Bagamoyo, pamoja na kupelekwa kwa miundombinu ya barabara na umeme katika maeneo hayo ya uwekezaji. Prof. Kitila amemhakikishia mbunge na wananchi wa Bagamoyo kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipa kipaumbele kikubwa eneo hilo na kwamba hakuna mwananchi atakayepoteza haki yake ya fidia. “Mheshimiwa mbunge nikuhakikishie serikali itaenda kulipa fidia na sasa tunakamilisha tathmini ili tuende kulipa fidia kwa awamu ya pili. Na mheshimiwa Rais hili ni eneo ambalo amelipa kipaumbele, lakini tumeweka utaratibu mpya kwanza TISEZA wenyewe kwenye mapato yao watatumika pia kulipa fidia. Lakini wawekezaji pia tunawashirikisha na serikali yenyewe. Kwahiyo wananchi wetu wa Bagamoyo wawe na uhakika haki zao haziwezi kupotea”, ameeleza Prof. Kitila.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 03 October 2026 16:57:14 GMT
3430
44
1
9

Music

Download

Comments

msangule12
Omary Msangule :
safi
2026-10-04 05:42:14
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About