@kibopa_farm: JOGOO AU TETEA? Wafugaji wengi, hasa wanaoanza ufugaji, huwa wanapata changamoto kutofautisha kifaranga wa kiume na wa kike. Katika video hii tunakuonyesha namna ya kumshika na kumchunguza kifaranga ili kupata viashiria vinavyoweza kukusaidia kutambua kama ni JOGOO au TETEA . KUMBUKA: Si kila njia ya kumtazama kifaranga inaweza kutoa uhakika wa 100%. Usimdhuru wala kumbana kifaranga wakati wa kumchunguza. Kwa mfugaji, kujua jinsia mapema kunaweza kukusaidia kupanga: • Idadi ya majogoo na matetea • Chakula na nafasi • Mpango wa uzalishaji • Mauzo ya kuku kulingana na mahitaji ya soko Tazama video hadi mwisho, kisha COMMENT: Wewe huwa unatofautishaje JOGOO na TETEA? SISI KIBOPA FARM-Tunafuga, tunafundisha, tunashirikisha uzoefu. #kibopafarm #ufugajiwakuku #poultryfarming #ufugajiwakisasa #poultryeducation