@kipunje: JIMMY MAFUFU Shetani ni mdanganyifu sana, tazama hapa familia nzima imetoka kumwabudu Mungu kwa upendo mkuu, lakini punde si punde Baba kachukua bastora kampiga mama kichwani, mama anaenda kuzikwa baba anaenda jela halafu watoto wanabaki wakihangaika bila wazazi na Mungu aepushie mbali kama ndugu waliobaki hawatakuwa na tamaa na kuwapora mali zao Siku moja niliwahi kupata mkasa mkubwa sana, kuna mtu aliujeruhi mno moyo wangu nikakasirika mno nikachukua panga nikasema leo namkata kichwa lakini kabla hasira yangu haijanizidia picha halisi ya watoto wangu ikaninia ghafla kichwani, nikakumbuka kwamba hawa watoto wangu hawana mjomba wala babu wala mama mkubwa wala mama zao ambao wamewahi kuwanunulia hata kalamu ya kuandikia shule, moyo wangu ukaniambia Mafufu ukienda jela hawa watoto watageuka ombaomba mtaani leo upo hakuna mtu anawatazama vipi siku ukiwa haupo? nikahuzunika sana nikaamua kuishinda hasira yangu na kudhamiria kuepuka kila hatari inayoweza kuniweka kolokoloni na kuwaacha watoto wangu wakitaabika Nataka kusema nini? Mnapoamua kuishi pamoja kama Mume na Mke ikifika wakati hamuelewani ni vizuri kuachana kwa amani, Yes yaweza kuwa ni usaliti na udanganyifu katika ndoa, ni kweli hayo yanaumiza mno lakini wanaume wenzangu msishindwe na hasira zenu bali yatazameni majukumu ambayo Mungu amewaamini na kuwapatia ambayo ni kutunza watoto wenu na kuwasaidia kuzifikia ndoto zao, mti mmoja akasema unakuta umelea na watoto na wamekua mwanamke anakwambia sio watoto wako je utajizuiaje? Ni kweli utapata maumivu lakini ni vizuri kujiondoa katika ndoa hiyo kwa amani kuliko kumuua mama wa hao watoto, kuna umri ukiufikia watoto sio lazima wawe wale uliomwaga mbegu tu bali kila mtoto anapaswa kuwa mtoto wako kama mzazi Mwisho hakuna ajuae nini kimesababisha maudhi haya mpaka mwezetu kumtoa roho mkewe lakini niwahusie dada zangu, Biblia inasema katika Mithali 18:12 Kabla ya uharibifu moyo wa Mwanadamu hujivuna. lakini anasema katika kitabu cha MITHALI 16:18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko Hayo maandiko hapo juu yatusaidie kuelewa namna tabia zetu zinavyoweza kuchochea uharibifu Pumzika kwa amani dada yetu na tunakutakia kila raheri kaka yetu kwa matokeo unayokwenda kukabiliana nayo baada ya kushindwa kuzuia hasira zako, mwisho kabisa Mungu awatunze watoto hawa ambao wazazi wao kimsingi hawajaona umuhimu wa kuendelea kuwatunza kinyume chake tofauti zao leo zimewagharimu pakubwa watoto wasio na hatia ACHA NIWE SINGLE TU MAMBEGHES
Jimmy Mafufu
Region: TZ
Sunday 04 October 2026 08:55:35 GMT
Music
Download
Comments
SIWA KIKALA :
Family umeongea sawa kabisa
2026-10-04 14:16:15
4
Pius Maduhu :
Big up mwamba, niko upande wa mwanamme mwenzangu
2026-10-04 12:29:18
36
Monique💫 :
usiwah kutamani maisha ya watu mtandaoni maisha ya ndoa magumu sana yanahitaji roho ngumu sana🥲 wazazi wetu walivumilia mengi sana🙌R..i.p. Mpendwa
2026-10-04 11:24:02
70
AgNes :
Inauma sna jamn[Crying][Crying]
2026-10-04 10:32:22
0
Juma Halifa :
mwamba nimemkubali safi sana
2026-10-04 15:12:15
2
Rachel Lameck :
Mimi naona ndoa ikiwa na Aman vita inakua kubwa sana 🥹🥹
2026-10-04 11:15:41
20
user2466766247716 :
Mali na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana
2026-10-04 10:40:16
17
shahadi :
Ndo maana mimi sasa hivi nawaogopa wanaume hata sielewi nitaishije
2026-10-04 13:02:17
11
Vera cosmetics 🧴 :
i choose peace over money🥰
2026-10-04 18:29:37
0
Machuwa 🎀 :
U said it all ❤️
2026-10-04 13:51:23
0
SAMAH💕 :
Daaaaah nikiangalia wanangu kuna wakat mm ndo napambana zaid kuliko baba Yao bc namuangalia tu kama naish na mtu nisiemjua Allah atupe busara na hekima kwenye hizi ndoa ila ndoa ni mtihan mkubwaaa Allah ampe kaul thabit huyu mama
2026-10-04 09:07:33
16
Love 😍 :
kwani lazima kuolewa jmn😢
2026-10-04 12:44:24
2
magreth564 :
very sad
2026-10-04 11:15:26
0
meeggy2 :
Watto bado wadgo dah 🙏
2026-10-04 11:55:35
0
winifrida :
sitaki ndoa narudia sikakiiiii ndoa jamani kwani lazimaaaaaaaaaaaaaaaa
2026-10-04 18:04:58
1
Tatu Hamza :
ee mungu duu inaumiza sana watoto Bado wadogo jaman watakao waangalia wawe na huruma juu Yao inaumiza sana leo wamegeuka kuwa mayatima😭😭
2026-10-04 09:49:14
5
Jay home store :
kuna muda mtu unatamani usiwe tajiri maana zikishakuja washauri ni wengi mnoo
2026-10-04 10:39:41
9
Chagga boy. :
makini sana mwamba.
2026-10-04 14:07:02
3
user9521386793477 :
naomba kujua Sheria ya kumiliki bastora Tanzania ni gan jaman, mbona kira mtu ni kama Yuko na bastora
2026-10-04 14:08:32
0
zanuri mkuvaja :
ndoa ni siri kubwa
2026-10-04 11:25:45
1
🦋 :
Ee M/Mungu!😭😭😭🙏🙌🙌🙌
2026-10-04 13:24:07
1
Cherry Banks🍒 :
Sa mtawaambia nini watoto
2026-10-04 12:08:57
2
Mamie Opratz :
Kwakweli mimi nasemaga naishi kwenye Ndoa kwaajili ya watoto wangu, so hasira inapotaka kuwaka na kunipa maamuzi ya ajabu hua nawaza wanangu nisipo kuwepo🙌🏼 Mungu tusaidie wanandoa, sio kazi rahisi
2026-10-04 14:40:55
4
themwibarafinest :
Wanaume Tusiache utamaduni wa kukutana na kuongea ya kwetu Kiume Ume
2026-10-04 14:18:04
1
prisla kilawila :
😭😭😭pumzika Kwa Amani dada rahaya mwanga WA milele uwangaziwe daima.
2026-10-04 11:40:04
1
To see more videos from user @kipunje, please go to the Tikwm
homepage.