@sirbeat.the.best: Taarifa imetumwa kutoka kwa Salim Mussa Omar Mbunge wa Jimbo la Gando kuhusu Raiyan Hemed Amour, mkaazi wa Kwale Mpona, mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza kutoka skuli ya Kizimbani Wete, amepatikana leo (Jumapili) akiwa amefariki kwenye kichaka huku akiwa amekatwa mkono akiwa na sare za skuli baada ya kutokuonekana tokea siku ya Ijumaa. Hakika huu ni uovu, uonevu na unyama uliopitiliza na ni katika mambo yasiyotakiwa kuvumiliwa au kufumbiwa macho hata kidogo ndani ya jamii yetu. Ni imani yangu kwamba Mamlaka husika kwa kushirikiana na wananchi watawatia nguvuni wale wote waliohusika na unyama huu. Natoa pole kwa familia ya Raiyan, waalimu na wanafunzi wa skuli ya Kizimbani Wete na jamii yote ya Kizanzibari. Namuomba Allah ampokee mja wake huyu hali ya kuwa amemridhia na kwa kitendo hichi cha kudhulumiwa iwe ni sababu ya kumsamehe makosa yake na amuingize ndani ya pepo yake tukufu, aamin. InnaliLlahi wainna ilayhi raajiun. #Zanzibar #viral #tanzaniantiktok🇹🇿 #clouds #Pemba
Allah Atujaalie Waja Wake Mwisho Mwema🤲🥹🙏 Ameen 🤲🥹🙏 Thumma Ameen 🤲 😭 🙏 🥹 💖
2026-10-04 15:59:14
0
Bab.saleh21 :
Uzuri ni kwamba dhulma haikopeshi..
Allahumma ghfirlaha warham ha waskanna fil jannah..🤲😔
2026-10-04 13:39:44
32
TÜRK 🇹🇷 :
Kifo ni mwisho wa safari ya duniani, lakini mwanzo wa safari ya Akhera. Tumuombe Mwenyezi Mungu atujalie mwisho mwema na atusamehe madhambi yetu. 🤲🏽🕊️
2026-10-04 13:17:24
23
saidinleee :
Mtot mzur anamalengo yake kibao wanakwend kumzulumu hiv hiv dah
2026-10-04 13:51:43
6
muba boy :
poleni
2026-10-04 15:44:30
0
Chande Habibu :
Alla ajaalie safari njema na amsamehe madhambi yake na umuunngize peponi kwa rehma zako yaAlla ww tu ndie mjuzi wa yote haya yiolio fanyika na ndie utae hukumu.
2026-10-04 14:05:31
7
user4028135814691 :
mungu atamlipa alofanya hv punzika Kwa amani mdg wangu SS tupo nyuma yako
2026-10-04 16:22:16
3
mima27sp :
Innalillah wainna ilayhi rajiun 🥹
2026-10-04 15:09:00
1
nameless🇧🇳🇹🇿🇰🇷 :
Shida ya wazanzibar hawataki watoto wao kufungwa hata kama kakutikana na kosa ukimfunga unaweka uhasama unaonekana una roho mbaya jaambo unaloliweza usimuachie Mungu ndio mana vitendo viovu vimeongezeka siku hizi watu hawaogop tena