@shukuru_media: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Elthon P. Banzi, amesema kampeni hiyo ni sehemu ya mikakati ya Jeshi la Polisi ya kupunguza vifo na madhara yanayotokana na ajali za barabarani, baada ya kubainika kuwa baadhi ya ajali husababishwa na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani. ACP Banzi amesema operesheni maalum ya kuwachukulia hatua madereva na abiria watakaobainika kutovaa kofia ngumu (Helmet) inaanza tarehe 05 Oktoba 2026, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utekelezaji wa sheria na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa matumizi ya Helmet. #ShukuruMedia #Zanzibar #PolisiZanzibar #Helmet #UsalamaBarabarani