@kusagatv: MWANAFUNZI RAIYAN HEMED AMOUR APATIKANA AMEFARIKI, MBUNGE AOMBA UCHUNGUZI Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Kizimbani, Raiyan Hemed Amour, amepatikana amefariki Oktoba 4, 2026, baada ya kuanza kutafutwa tangu Ijumaa, huku akiwa amekatwa mkono. Raiyan, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Jimbo la Gando, Zanzibar, amepatikana katika mazingira yaliyomshtua Mbunge wa Jimbo hilo, Salim Mussa Omar, ambaye amelitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo na sababu ya kifo hicho. Mbunge huyo ametaka hatua kali zichukuliwe iwapo wahusika watabainika, huku akitoa pole kwa familia na wananchi wa Jimbo la Gando, hususan wakazi wa Kwale Mpona. Ameiomba jamii kuwa macho na kutoa taarifa kwa mamlaka za usalama pale hali ya taharuki inapotokea. “Naomba wananchi tuwe macho sana, hii dunia imegeuka. Sikuwahi kushuhudia mambo haya nikiwa mtoto ila leo yanajitokeza, si jambo la kawaida hata kidogo,” amesema Mbunge huyo.
MWANDISHI WA WANANCHI
Region: TZ
Sunday 04 October 2026 14:25:16 GMT
Music
Download
Comments
Rahma Said 🥰♥️ :
mimi najiulizaga wanaoua watoto wanakuwa wamewakosea nini??au visasi juu ya wazazi wao?!au ni nini haswa 🥺🥺🥺🥺
2026-10-04 15:41:43
82
twalha :
it's sad
2026-10-05 07:07:21
0
𝒏𝒂𝒔𝒓𝒂 🇹🇿 :
𝒑𝒐𝒍𝒍𝒆𝒏 𝒔𝒂𝒏 𝒅𝒖𝒉
2026-10-05 06:24:55
0
عبدل barri :
Aaaàah Zanzibar mbona izi tabia hazishiiii why why..??🙏😭😭😭
2026-10-05 03:14:07
0
habbty jassy :
Allahumma ghufir laha warhamaha waskanhm fill jannah[Pleading][Pleading][Pleading][Teary eyed][Teary eyed]
2026-10-05 05:44:51
0
Mrs Ibrahimu og. :
Mwenyezimungu amlaze mahala pema pepon🤲🤲🤲🤲🤲🤲🤲
2026-10-04 16:33:24
107
subiraomar151 :
mola amlaze mahala pema peponi aaami
inahuzunisha sana doh mola awalinde watoto wetu
2026-10-04 15:40:38
42
Asia :
Mungu ampokee ampe kauli thabit insha allah
2026-10-04 16:37:07
51
miss_naj7𐙚 ̊ᥫ᭡⭑ :
shida inaanzia kwenye miundombinu🥺watoto wanatoka kwale wanasoma skuli ya kizimbani ukizingatia njia sio salama wanapita mabonde kwa mabonde, na njia inayopita miusafiri hakupatikani boda boda wala bajaji kwamba mtoto atapanda atoe nauli hakuna na ni kwasababu ya ndio ni mbovu kwaiyo inawabidi wakate mabonde ndio waifike shule. kwaiyo serekali ingetengeneza shule ya msingi na secondary kwale na bara bara ikawa nafuu hii inasaidia kdg kwa usalama wa watoto IMAGINE hilo ni tukio la nne ambalo yanafanana na yanatokea hapo hapo eneo hilo hilo, na watoto wote wa kwale wanaosoma kizimbani washasema hawaendi tena skuli wanaogopa je itakuaje kuusu watoto? kiukweli mji wa kwale miundombinu mibovu na ndio mana matukio haya na yake ya ukatili. 😭😭🙌💔allah atupe subra
2026-10-04 19:16:24
43
Aqay🌹🥰 :
daah sikuhiz mtu akipotea kupatikana akiwa hai ni ngumu , sijui. tunaelekea wapi jaman Mwenyez Mungu atuokoe na hili janga
2026-10-04 15:05:50
148
Dirtymoney@430 :
it's sad
2026-10-05 03:05:54
1
Nasy♉️ :
she is very beautiful ,innalillah wainna ilayh rajiun
2026-10-04 16:56:06
22
mashaallahyusrafashion_2 :
ALLAH AWAPE SUBRA WAZEE WAKE 😭😭😭
2026-10-04 15:45:32
32
kizzystrem :
awaja mbaka kwer watu sio wema
2026-10-04 16:18:16
5
Somoe Amani :
Subuhannaullah Allah anawaona waliofanya ivyo
2026-10-04 14:59:44
15
karimukawaya :
mungu amlaze mahali pema peponi amin
2026-10-04 16:47:00
7
Gucho saka :
DUNIA ingekua gari ningeomba kushuka
2026-10-04 18:50:24
6
Rellah🎀 :
halafu karembo mashallah wamemkatishia ndoto zake😥😥
2026-10-04 19:48:35
5
Salha Chumi :
😭😭😭eeh Mungu wewe wajua 😭😭muondolee adhabu ya kabri mwanao yaraby
2026-10-04 22:00:15
0
NDESA💢 BOY :
Maisha ya duniani ni mafupi sana unapo kuwa hai na bado una pumua ni jambo la kumshukuru allah yeye mbele yetu sisi nyuma yake allah amsamehe mazambi yake na amjalie kila lenye kheri kati yake😭🥹
2026-10-04 21:01:22
2
Official&CHWRY@BOY23% :
Dah namjuwa uyu n madad zake mapacha.
Allah amuondolee adhabu na amsamehe n sisi atusameh madhamb ya siri na dhahir
2026-10-04 20:23:20
3
Muthayra :
Allah amtilie nuru kwenye kaburi lake 🥹daah imeniuma sana maumivu hayo ni ya mda kusahaulika allah awatie nguvu wazee wake sio kwa maumivu haya 🥹🥹
2026-10-05 05:42:49
3
tatu moo :
mungu amlaze mahali pema hana hatia mtoto wa watu maskini ya mungu inauma dah so vzr jmn wl so ubinadam kwa kweli 😭😭😭😭
2026-10-05 06:22:52
1
Juma muhanji :
kwaiyo zanzibar nao wanataka kushindana na Arusha
2026-10-05 05:36:31
0
To see more videos from user @kusagatv, please go to the Tikwm
homepage.