@aviationswahili: Ndege aina ya Embraer 120, yenye usajili 5H-HLL, imeripotiwa kutua kwa tumbo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo, Oktoba 4, 2026. Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mashahidi wa tukio hilo, ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu katika mfumo wa magurudumu ya kutua (landing gear), hali iliyosababisha kutua bila magurudumu kushuka kama ilivyotarajiwa. Tukio hilo linadaiwa kutokea majira ya saa 4:00 hadi 5:00 asubuhi, ambapo vikosi vya zimamoto na uokoaji vilikuwa tayari eneo la uwanja kwa ajili ya kuchukua hatua za dharura na kuzuia madhara zaidi. Ndege hiyo iliondolewa muda mchache baadae na haikusababisha usumbufu mkubwa kwa safari za ndege nyingine. Kwa sasa, Mamlaka ya uchunguzi wa ajali za anga "Tanzania Civil Air Accident Investigation Branch (TCAAIB) imeanza uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha hitilafu na mazingira yaliyopelekea ndege hiyo kutua kwa tumbo. Taarifa zaidi kuhusu hali ya ndege, abiria na wahudumu pamoja na matokeo ya awali ya uchunguzi yanatarajiwa kutolewa na mamlaka husika, ingawa taarifa za watu wa karibu walioshuhudia tukio hilo zinasema hakuna watu waliojeruhiwa.
AVIATION MEDIA
Region: TZ
Sunday 04 October 2026 14:54:05 GMT
Music
Download
Comments
@𝐈𝐭𝐬.𝐑 𝐄 𝐔 𝐁 𝐄 𝐍 😎 :
Respond ya hao jamaa sasa ni 30min later😂😂😂 hii ndo bongo.
2026-10-04 16:42:47
0
Moresby William :
kumbe ndege zina matumbo mlikuwa hamsemi[Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-04 17:55:48
1
user4084567284619 :
sasa fire badala afate anasubili ilipuke hii nchi imelaaniwa
2026-10-04 16:25:20
14
Nderingo :
Uwanja wenyewe kama pori ndege ikilipuka utashika moto kama mbuga
2026-10-04 16:44:15
10
Its_Natrix :
Belly landing 🛬
2026-10-04 18:30:41
0
Shamsi Maarifa :
🤣🤣🤣🤣🤣ndo hii wametengeneza mafundi wetu🤣🤣🤣🤣
2026-10-04 16:05:03
3
Antananaariwowo :
Sasa hawa Fire badala ya kuifuatilia nyuma nyuma kama tunavyona kwenye nchi nyingine wao wamesimama tuu!
2026-10-04 18:45:21
1
Laura Rock :
Tumbo la mwanamke au mwamume????
2026-10-04 18:30:47
0
Www.Daudi msangi.390 .Arusha . :
ruban hajachomoa Tair nn
2026-10-04 18:08:32
0
Shija :
kwan inatakiwa itue kwa kichwa?
2026-10-04 16:55:46
0
Don Jay :
WATU WA ZIMAMOTO WALILALA ZAO HOI[Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-04 17:04:55
0
octavia🧚♀️🧚♀️ :
ndo maana naogopa kwanza huku mitaani zinapita chin mpaka unatoka nnje😳😳😳
2026-10-04 17:53:55
2
~~de mapunda jr ☠️ :
msipende kilaumu fire 🚒 Kuna kanuni na taratibu za kunidil kama ndege ikitulia tumbo
2026-10-04 17:52:16
1
noel wilfred njau :
apo ndani kivumbi
2026-10-04 18:56:18
0
Maya Mayna :
sasa hilo ni vumbi 😳😳au maji😁
2026-10-04 18:16:18
0
Iddi Rahim :
kia
2026-10-04 17:25:17
0
hamydebrazilian1 :
dah hope wako salama
2026-10-04 18:15:09
0
Naj✨ :
Kwan huu uwanja KIA uko kwa wap 😂😂😂 tunaoujuaaa haupo ivo
2026-10-04 17:44:35
0
💫spak boy :
noma mzee
2026-10-04 18:57:53
0
Paul Wagine :
Zimamoto hapo walikuwa Tiktok
2026-10-04 18:00:05
0
Henry :
na trekta lilikua linafanyaje kwa airstrip
2026-10-04 18:56:51
0
FLAS GOLD :
fire
2026-10-04 17:01:43
0
Zita :
Hii sio kia boya ww
2026-10-04 18:10:26
0
timmztraveller :
Anaetoa taarifa kama kanywa highlife
2026-10-04 18:23:58
0
cashmadame938 :
😁😁😁😁
2026-10-04 17:45:26
0
To see more videos from user @aviationswahili, please go to the Tikwm
homepage.