@its_mtana: Alhamdulillah🙏,leo moyo wangu umeguswa kupita maelezo😒🥹. Kwa niaba ya @Hijab Girls Tanzania kama Afisa Habari, leo nimepata bahati ya kutembelea Kituo cha Watoto Walemavu na Wasiojiweza kilichopo TEGETA WAZO, Sikuwa naenda tu kuwatembelea, nilikuwa naenda kujifunza... lakini nilichokiona kimenifundisha maana halisi ya ujasiri, upendo na matumaini. Watoto pale ni malaika,Wanatabasamu licha ya changamoto kubwa wanazopitia. Wengine hawatembei, wengine hawaelewi chochote, wengine hawawezi kuongea vizuri... lakini mioyo yao ni safi kuliko sisi. Tabasamu lao moja tu lilinifanya machozi yanitoke. Ukweli ni kwamba, *HAWA WATOTO WANATUHITAJI SANA.* Wanahitaji upendo wetu, kama kauli mbiu yetu isemavyo “UPENDO WETU ,TABASAMU KWAO” ,Wanahitaji chakula, mavazi, matibabu, elimu, na zaidi ya yote - KUTIWA MOYO kuwa na wao bado ni sehemu ya jamii yetu. Wasimamizi na walezi wanajitahidi sana, lakini mzigo ni mkubwa, hawawezi peke yao. Ninawaomba ndugu zangu, tusiwageuze kuwa takwimu tu. Ni watoto wetu. Ni ndugu zetu. Leo nimejionea kwa macho yangu jinsi support ndogo kutoka kwetu inavyoweza kubadilisha siku tulichoweza, lakini safari ni ndefu. Naomba yeyote anayeguswa na hii, tusaidiane. Hata dua yako, hata share ya hii video, ni msaada mkubwa sana. Mungu atubariki sote na atujaalie kuwa sababu ya furaha ya wengine. Ukitaman kuungana na sisi unaweza kututumia jumbe DM kwa maelekezo zaid❤️🥹🫂@Ms ~Mtana8 *#HijabGirlsTz #TegetaWazo #WatotoWenyeMahitajiMaalum #Tusaidiane #

its_Mtana ❤️🫂
its_Mtana ❤️🫂
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 04 October 2026 14:55:55 GMT
4726
469
13
23

Music

Download

Comments

nunu_classiccollection
nunusuley :
Mashallah ❤️❤️❤️Allah akulipe na awalipe khery nyote mloanzisha hiv vikundi na kuvifanyia kaz ,kuna wengi wanapitia changamoto watu hawajui ila mnafungua watu waone ni yapi watu wanapitia na kuwapa watu chachu ya kuzid kutoa Swadaqa na kusaidia wenye uhitaj🥲🥰......Allah awalipe inshaallah hili ni kubwa
2026-10-04 19:02:13
2
lildatz
lil_ommie :
Jazakalllahu khaira
2026-10-05 04:17:37
1
umm.ghaniyath3
umm ghaniyath :
nakupenda sana we DADA Allah akuhifadh always
2026-10-04 15:48:13
2
halimaamily258
Halima Amily :
naomba niwe upand wapili wako
2026-10-04 20:18:17
1
zaira.cute6
ms zayra😜 :
Mashaallah♥️Allah akupe moyo hiohuo daima🥰🥰
2026-10-04 16:43:15
1
officialnajma.03
Officially najma :
Mashallah mungu akunze
2026-10-04 17:57:13
1
fatma.mohammed0937
Fatma Mohammed :
2026-10-05 05:38:08
1
perfume_paradise_stylish
PERFUME_PARADISE_STYLISH :
Allah atubless tuikamilishe na hii🥹🤲
2026-10-04 15:15:18
0
da.smyle3
da smyle😊 :
kipo wapi hiko kituo
2026-10-04 14:59:24
0
ayshanaty
@yshanaty❤️ :
Mashallaah ❤️Allah akujaze khery na Baraka telee Habbty lnshallaah 🤲🏼
2026-10-04 16:09:08
0
asiamustafa24
Asia🦋 :
❤️❤️❤️
2026-10-04 16:05:39
0
waziri.hurra
Waziri Hurra :
❤️❤️
2026-10-05 04:19:43
0
To see more videos from user @its_mtana, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About