@uwazi.online.tv: SSP DKT. KYOGO: WAUMINI WA DINI TUSHIRIKIANE KUDUMISHA AMANI NA USALAMA. Waumini wa Kanisa la Mbingu Duniani lililopo Engutoto, mkoani Arusha, wamepatiwa elimu kuhusu nafasi yao katika kuhamasisha amani, usalama na kukemea vitendo vya uhalifu katika jamii. Elimu hiyo imetolewa leo Oktoba 4, 2026, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya “Arusha Salama.” Akitoa elimu hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Dkt. Ezekiel Kyogo, akiambatana na wasanii mbalimbali kutoka kitengo cha ushirikishwaji wa Jamii, Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu Dodoma, amewataka waumini wa dini kutumia nafasi yao katika jamii kuhamasisha amani na usalama, kukemea vitendo vya uhalifu pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu. SSP Dkt. Kyogo amesisitiza pia umuhimu wa waumini kuwa wazalendo kwa Taifa lao na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kujenga jamii yenye amani, utulivu na usalama, akieleza kuwa viongozi na waumini wa dini wana nafasi kubwa ya kufikisha ujumbe wa amani na maadili kwa jamii. Elimu hiyo imetolewa kupitia burudani kwa wakazi wa Engutoto, mkoani Arusha, ambapo wananchi wamehamasishwa kushiriki kikamilifu katika masuala ya usalama na kudumisha amani katika maeneo yao. Zoezi hilo ni sehemu ya kampeni ya “Arusha Salama” inayotekelezwa kwa kushirikisha jamii katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu.#polisitanzania #uwazionlinetv
uwazi online tv
Region: TZ
Sunday 04 October 2026 19:56:21 GMT
Music
Download
Comments
Lauking255 :
mkali ana vybe balaa toop
2026-10-05 09:33:12
0
Salha Mhina :
wapi Geoff ❤️❤️❤️❤️❤️
2026-10-05 08:18:19
0
user2099369018288 :
Mungu awatunze.Mungu ni wetu sotee🥰
2026-10-05 06:24:49
2
Dr of chemistry🇹🇿 :
yuhu polisi inaoneka kwenye chenja alikuwa vizuri
2026-10-05 15:16:14
0
user1707672202252 :
hapo wanatangaza amani huku wameficha mapanga
2026-10-05 12:57:03
1
Asante Milinga :
👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
2026-10-05 12:15:36
0
triiz :
wooo wapiiii mbing dunian
2026-10-05 15:07:46
0
macky :
YESU umestahili
2026-10-05 13:50:43
0
Joshua ben Paul JP :
Napenda sana askari wacha Mungu.
2026-10-05 11:37:30
0
user10401539965817 :
nikiona hiii nasikia uchungu sana kwenye moyo wangu mungu atusaidie sana
2026-10-05 09:25:29
0
mr sirro :
wap mapunda mtu wa vibe 🥰
2026-10-05 10:19:10
0
abgael :
hakika mungu ni mwema
2026-10-05 09:03:18
0
Jacklini Sanare :
Ee mwenyez Mungu waongozw
2026-10-05 08:09:29
0
Zawad Halidi :
ameen kuwa na hofu ya mungu ni raha
2026-10-05 09:21:23
0
Mmasue :
wapi huko nikuje niunganike jamani
2026-10-05 07:54:52
0
user1707672202252 :
ccm oyeee
2026-10-05 12:54:53
0
Alex Mosha :
wanadhani tutasahau 29/10
2026-10-05 05:07:04
0
Ismail Francis :
Namkataa shetan na mambo yake yote
2026-10-05 09:22:45
0
LOVE CHAR'S🫶 :
wahumini wa mbingu duniani hawakogo hivi kwenye kipindi cha sifa bhana wamepoa sana,
sema nn hawa police wasituzuge 🤣🤣🤣
2026-10-05 13:40:48
0
starborn447 :
Wametambua makosa yaoo wanajaribu kurudi kwenye jamiii
2026-10-05 10:51:24
0
wisperfect :
hicho alichovaa askari ni nini
2026-10-05 07:21:44
0
useMwl kelvin shao :
aiseeee tunawadai roho nyingi sana
2026-10-05 11:25:19
0
Dotto Nasari :
🥰🥰🥰
2026-10-05 11:16:43
0
To see more videos from user @uwazi.online.tv, please go to the Tikwm
homepage.