@jambotv_: VIDEO: Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa(Bulldozer) amesema bilionea wa Zimbabwe marehemu Wicknell Chivayo alipiga simu kwake akitaka kuhudhuria mkesha lakini alimkatalia. Mwamposa amesema hayo katika ibada ya jumapili iliyofanyika kanisani kwake Kawe akieleza kuwa alimkatalia Chivayo kwa sababu aliona kuwa kama angekuja basi watu wangenasibisha jambo hilo na siasa lakini pia aliogopa kwamba watu wangedhani fedha zote za kanisa hilo zinatokana na tajiri huyo. Ameeleza kuwa Chivayo aliendelea kupiga simu lakini alikataa kupokea simu zake kutokana na hofu aliyokuwa nayo. Pamoja na hayo amedai kuwa tajiri huyo alikuwa akiishi maisha ya kifahari na gharama kiasi ambacho hakuna ambaye angedhani kwamba atakufa siku moja