@innocent_raphael: Kuna hoja ya Mbunge iliyowahi kuzua mjadala kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto ya watumishi wanaohama vituo vya kazi, hasa maeneo ya pembezoni, ambako baadhi ya watumishi wanapangiwa lakini hawadumu kwa muda mrefu. Hoja iliyotolewa ilikuwa kwamba watumishi wa kike waolewe ili waweze kubaki kwenye maeneo wanayopangiwa, badala ya kuendelea na changamoto ya kuhamahama kutoka kituo kimoja kwenda kingine. Hata hivyo, nyuma ya kauli hiyo kuna tatizo halisi linalohitaji kuangaliwa kwa upana zaidi, kwa nini mtumishi anapangiwa eneo fulani, lakini anapofika anaanza kutafuta namna ya kuondoka? Katika Bunge, Serikali yenyewe imewahi kukiri kuwa watumishi, hususan walimu katika maeneo ya pembezoni, huwa na hamu ya kuhama kwenda mijini. Miongoni mwa hatua zilizotajwa ni kutomtambua mtumishi kuwa na sifa ya kuhama kabla ya kutimiza angalau miaka mitatu katika kituo alichopangiwa. INAENDELEA.... #siasa #innocentraphael #innocentraphael #tanzaniantiktok🇹🇿
Innocent_Raphael
Region: TZ
Monday 05 October 2026 06:38:40 GMT
Music
Download
Comments
the_universe_princess🥰 :
oooh😂 WATAMISEMI SIE
2026-10-05 10:57:11
0
Tension clamp :
kama hukuwa nampenzi kwisha habari
2026-10-05 08:58:12
18
joleen jacecho :
hivi anapajua huku kigoma[Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-05 08:23:27
18
Po-shie💜 :
Siolewi na nitahama😂😂😂😭😭😭
2026-10-05 09:15:49
10
Shariah :
😂😂😂😂 Kaz tunayo ko saiv ni kuolewa na viongoz wa mitaa nachoka mie
2026-10-05 10:07:19
5
Disminder Girl 😘 :
Tuolewe wapi, na Nani, na nini, na vipi, mmmmm Tamisemi 🤣
2026-10-05 09:56:24
2
A.mass :
mwanao ataajiriwa tu, tunza hii clip
2026-10-05 10:18:01
2
ka2gal♉ :
Niolewe na mnyakyusa alf wa Kyela 🥺
2026-10-05 09:53:40
2
PASCHAL MODOY :
hasa manesi Hali ni mbaya
2026-10-05 08:28:56
12
fau amani :
kwa mfano uku Makete uku mheshimiwa ach a mazarau
2026-10-05 08:30:24
14
Lorry@ :
Kuna ukerewe visiwan huku so tanzania kbs ni bc tamaa tu za watu wetu wa zaman🥺
2026-10-05 09:30:11
5
2baba :
ME NAONA IWEKWE SHERIA MTUMISHI AKIAJIRIWA APEWE MIAKA MITANO AWE AMEPATA MWENZA WAKE😁
2026-10-05 09:28:25
7
Ziada Kandanga :
Ajira zenyewe wanachelewa kutoa,mtu anamaliza chuo anakaa mtaani anapata familia yake akipata kazi vijijini unataka aolewe amuache mme wake
2026-10-05 10:29:38
1
LifeThread :
kama hakuna aliyempenda hapo kwa hiyo asiolewe sio?
2026-10-05 08:12:44
10
Lovey🥰 :
sa tunaolewa na nan kila mtu anamtu wake TAMISEMI FOR LIFE 😂😂😂
2026-10-05 10:41:41
0
Anny💕💌 :
Niko mbulu kwahy au basi wasije nitukana🤣🤣🤣🤣🤣
2026-10-05 10:57:03
0
mom adrii :
kaz kweli unajua madhara ya kuwa na pair Kijijin jamii haikuheshimu
2026-10-05 08:24:17
8
Po-shie💜 :
Sasa niolewe na nani uku🥺🥺
2026-10-05 09:16:06
5
Winfrida Gama :
hatuki mitara KIJIJINI mitara
2026-10-05 08:41:37
7
white diamond rey :
2026-10-05 10:10:26
0
salma :
Unatulazimisha tuolewe wapiiii
2026-10-05 09:00:29
2
Ney🦋 :
nina mume mkoa mwingine,sasa mnataka niolewe mara ngapi....namfata mume wangu bhn niacheni
2026-10-05 09:53:55
0
phina_ :
huku vijijini unapajua kweli
2026-10-05 09:14:38
3
GOOD MAN :
ndo anacho fikiria
2026-10-05 09:16:49
2
Urbanstitch_5 :
hatutaki bhn😂😂
2026-10-05 08:25:17
3
To see more videos from user @innocent_raphael, please go to the Tikwm
homepage.