@cawabemedia_: Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wamemlilia Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, kuhusu mwenendo wa bei ya ununuzi wa zao hilo katika msimu wa kilimo wa 2025/2026, huku wakisema bado hawajapata taarifa za bei ya pembejeo kwa msimu mpya. Wakulima hao wameeleza changamoto hizo Oktoba 3, 2026, wakati wa kikao maalum cha kusikiliza na kutatua changamoto zao. Wamesema msimu uliopita walilazimika kuuza tumbaku kwa bei iliyokuwa chini ya bei elekezi ya Serikali ya dola 1.95 kwa kilo, hali waliyoeleza kuwa imeongeza mzigo wa gharama za uzalishaji na maisha. Akijibu malalamiko hayo, Waziri Chongolo amesema ndani ya siku 10 atakutana na wataalamu wa sekta ya tumbaku pamoja na wadau wengine ili kupitia changamoto hizo na kutafuta majawabu yatakayosaidia kuboresha hali ya wakulima. Aidha, amewahakikishia wakulima kuhusu upatikanaji wa pembejeo kwa msimu mpya. Kuhusu madai ya baadhi ya kampuni za ununuzi wa tumbaku kuwa na madeni kwa wakulima ambayo hayajalipwa tangu msimu uliopita, Waziri Chongolo amezitaka kampuni hizo kuhakikisha zinalipa fedha wanazodaiwa wakulima ndani ya siku 30, ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kilimo.
cawabemedia
Region: TZ
Monday 05 October 2026 07:32:29 GMT
Music
Download
Comments
maiko msigwa :
Hii idara bashe alikuwa anaijulia
2026-10-05 12:43:19
6
richardbasu1 :
@tiktokers
2026-10-05 14:05:04
1
Mchikatheone :
hii nchi wakulima tunaonewa kila upande yaani
2026-10-05 08:09:33
8
kaka wa chunya✓🦅 :
icho kilimo Cha tumbaku kina mateso mungu nipe akiri mpyaa nisije kufkilia tena kuludii kwenye icho kilimo mungu baba
2026-10-05 19:29:06
1
deogratiusleonard2 :
bashe alikuwa anafatilia vizuri akatolewa
2026-10-05 13:41:21
4
user9166239771618 :
LAKINI TUKUMBUKE KWAMBA KILAKITU NI CHA CCM CHAMA CHA MA
2026-10-05 15:03:06
3
Steve mnyamwezi :
hiyo ndo tanzania mzee shida ni,uongozi wajuu kuto jali
2026-10-05 14:11:23
3
qis :
mtamkumbuka Bashe
2026-10-05 13:30:54
2
msuyaugweno777 :
endeleeni kuomba mungu hata hill litapita
2026-10-05 14:19:14
3
@komanya76 :
kwan kulima tumbaku ni lazma, mbona sis Kanda ya ziwa pamba tumepga chin😂😂😂
2026-10-05 13:45:59
3
bujikusimon :
hii video inanitoa machoozi
2026-10-05 13:02:12
1
Herman Willson :
😂ccm Mungu anawaona
2026-10-05 13:03:13
1
Kihiga :
Tutamkumbuka Bashe
2026-10-05 18:28:29
0
@kahama_free_market :
inabid mkuu ufuatilie hii habar mpka mwisho maana mwaka huu watu wamefilisika sana fuatilia hii inshuu
2026-10-05 10:59:33
1
Seif Mpwanda :
uko kusini Lindi na Mtwara mtu anakoma msimu mzima shamba alafu zao anaenda kopesha alafu bei anapanga aliokopa
2026-10-05 12:01:01
1
Aniseth Gama :
selikal tnawaomba mtusaidie kwahili maana inaumasana jamani kaziyatmbak ningumu sana huo wastani walonnua niwakm kandamiza sana mklima
2026-10-05 13:31:42
1
Erick 🐠🐠🇹🇿🇹🇿 :
nikweli dah
2026-10-05 11:58:50
1
user9166239771618 :
CCM 5 TENA
2026-10-05 15:02:02
1
Joshua $ Joely :
majibu yanayo tolewa hayaendani na wakulima wanavyo umiya
2026-10-05 16:46:37
0
Stanley Myombe :
Haya maisha yanaumiza sana, ukiwaza na Elinino ndio baaasi. poleni wakulima wa Tumbaku Tz.
2026-10-05 19:44:36
0
suzanampanda :
Endeleeni kumuachia Mungu 🙏
2026-10-05 18:41:59
0
user5088516003697 :
tuna mtaka hussein bashe
2026-10-05 19:34:15
0
mtawajr1 :
umeyapata kwa nn hukuwaita kabla acha kutuchanganyaa
2026-10-05 18:17:54
0
Linus Chagawalye :
haisaidii kitu hata mkilia machozi ya damu
2026-10-05 18:57:47
0
mkapachizo :
paza sauti 😭😭😭😭😭
2026-10-05 12:28:09
1
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm
homepage.