@openonlinemedia: JESHI la Polisi Mkoa wa Njombe limetoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani akiwa katika mvutano na dereva wa lori. Picha hiyo imeibua mjadala miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku baadhi wakitaka kujua chanzo cha mvutano huo pamoja na mazingira yaliyosababisha askari huyo kuonekana akizozana na dereva wa lori. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, leo Oktoba 5, 2026, jeshi hilo linafanya uchunguzi kupata taarifa zinazojitosheleza kuhusiana na tukio hilo. Jeshi la polisi limerai wananchi kutojichukulia sheria mkononi. #Pakua App ya #OpenMedia playstore kusikiliza #DoubleORadio na kutazama #OpenMTV au kupitia tovuti #openmedia.co.tz, Kwa Matukio, Habari na Matangazo wasiliana nasi 0677107271 au 0677107273.