@ishi.leo: 🔥 KISUKARI? USIPUUZE DALILI ZAKE! 🔥 Kisukari ni ugonjwa unaotokea pale kiwango cha sukari kwenye damu kinapokuwa juu kuliko kawaida. Kikidhibitiwa vibaya, kinaweza kuathiri viungo mbalimbali vya mwili. 🩸 KISUKARI NI NINI? Ni hali ambapo mwili hautengenezi insulini ya kutosha au hauitumii vizuri, hivyo sukari hujikusanya kwenye damu. 🚨 DALILI 5 ZA KUZINGATIA ✓ Kukojoa mara kwa mara ✓ Kiu kupita kiasi ✓ Kuhisi njaa mara kwa mara ✓ Kupungua uzito bila sababu ya wazi ✓ Uchovu na kuona ukungu ⚠️ MADHARA YA KUPUUZA KISUKARI ✓ Uharibifu wa figo ✓ Matatizo ya macho na kuona ✓ Uharibifu wa mishipa ya fahamu ✓ Kuongezeka kwa hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ✓ Vidonda vya miguu kupona kwa shida 💡 USHAURI MUHIMU: Kama una dalili hizi au una hatari ya kupata kisukari, pima kiwango cha sukari kwenye damu na pata ushauri wa mtaalamu wa afya. Usisitishe dawa ulizoandikiwa bila ushauri wa mtaalamu. 📲 Kwa ushauri na mawasiliano zaidi: Piga simu moja kwa moja au WhatsApp: +255723910488 🌿 UTAJIRI WA KWANZA NI AFYA YAKO MWENYEW AFYA NI MTUNZAJI WA MAISHA YAKO ITUNZE KILA SIKU! #ishileo #usa🇺🇸 #georgia #kenyantiktok🇰🇪 #afya