Lab Tech💉🩸💊🇹🇿 :
shida sio kuzaliana shida n watu kukimbia wilaya yao, hapo inabidi tujue kwann vijana wanakimbia na kuanzisha familia mikoa mingne kama Mbeya, DSM, Tunduma, Dodoma, Iringa nk, sasa hapo inabidi tuwe na 5 whys sytem, Watu ni wachache kwanini,,.? kwasababu vijana wanahama, kwann,,.? kwasababu Hakuna mzunguko wa hela, kwann hakuna mzunguko wa hela,,.? kwasababu hakuna viwanda na uwekezaji, Kwann hakuna viwanda na uwekezaji,,,.? Kwasababu miundombinu haijakaa sawa hasa barabara ya makete Mbeye, Jiografia ya makete, nk kwahyo cha msingi n kuifungua makete kibiashara ili baadhi ya vijana wajiendeleze wakiwa kwenye wilaya yao, Tuna mbao nyingi lkn hakuna kiwanda hata cha stiki, tuna mifugo mingi lkn hata yougurt tunanunua Njombe, apo cha msingi n kuifunguq wilaya kiuchumi watu wa makete wanazaliana sana tu, Kwahyo muheshimiwa tunaomba msaada wa kutufungulia wilaya tukianza na barabara ya makete mbeya, then tuanze kutafuta wawekezaji Ahsante
2026-10-06 16:30:40