@murally006: Kukimbizana na maisha bila kuwa na roho ya shukrani ni kama kunywa maji ya chumvi; kila unavyozidi kupata, ndivyo unavyozidi kuona una kiu na unakosa amani. Kutosheka na kile Mungu alichokujalia leo haimaanishi uache kupambana au uache kuwa na malengo makubwa. Inamaanisha unachagua kufurahia hatua uliopo sasa hivi huku ukijenga kesho yako kwa nidhamu. Anza siku yako kwa kuangalia baraka ndogo ndogo zilizokuzunguka,pumzi, afya, na utulivu wa akili. Hapo ndipo utajiri wa kweli unapoanzia. ☕💛🕊️ #gratitude #shukrani #swahilitiktok #mindset #innerpeace