@jambotv_: VIDEO: Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Aggrey Mwanri, amesema inawezekana katika uchaguzi uliopita kulikuwa na baadhi ya mapungufu, lakini amewataka wadau wa siasa kukaa pamoja na kuyajadili kwa mazungumzo ili kubaini yaliyokwenda vizuri na maeneo yanayohitaji maboresho. Mwanri amesema baada ya uchaguzi, ni muhimu vyama vya siasa kuangalia masuala mapana yanayolihusu taifa, ikiwemo uwekezaji, elimu, miundombinu na huduma za afya, badala ya kubaki katika tofauti za kisiasa. “Inawezekana kabisa katika jambo kubwa kama hili la uchaguzi kuna mapungufu yanaweza kujitokeza. Kuna mambo ambayo mtu akaona hayakuenda vizuri. Sisi tufike mahali tuketi wote kwa pamoja, tuzungumze na tuseme hili lilikwenda vizuri, lakini hili tunalirekebisha.” amesema Mwanri. Amesema mazungumzo na maelewano kati ya vyama ni muhimu kwa mustakabali wa taifa, akieleza kuwa mazingira yenye kutokuelewana yanaweza kuathiri hata imani ya wawekezaji katika nchi.
Jambo TV
Region: TZ
Wednesday 07 October 2026 09:54:22 GMT
Music
Download
Comments
mnyonge :
comedy time😏
2026-10-07 17:05:34
6
Nature is life :
Nchi inahtaji watu kama wewe
2026-10-07 17:45:14
9
elibarikijohnson9 :
Daniel 12:3
2026-10-07 15:40:31
1
Mashaka Shija :
ww ni rais wa kesho
2026-10-07 13:28:04
9
JOSEPH LOGOLIE :
acha comedy
2026-10-07 11:02:06
7
Mr. jerusalem :
tulisema kabla ya uchaguzi tuzungumze mambo hayapo sawa hamukutaka leo yameshatokea munata
2026-10-07 11:35:50
12
Paul :
kumekucha
2026-10-07 10:01:24
6
Otieno :
mtu anabadilika kutokanana mazingira
2026-10-07 10:54:11
5
Triple R :
Sio kwa ccm ni wanafki
2026-10-07 11:02:32
11
MWANA MPOPONGA FAMILLY :
apo alikua anamanisha vyama vyote vipeleke wabunge ili bungen papitishwe shelia zenye haki
2026-10-08 09:15:28
1
LFM. QUALITY SHOES :
umeanza kazi babu yetu.
2026-10-07 17:54:53
4
uninteme :
komedi
2026-10-07 10:21:11
5
g'father :
mzungungumze nini wakati mnakuwa tayari mmeisha jipa madaraka kama ni mazungumzo yawe hapajafanyika kabla
2026-10-07 11:55:33
2
emmanuel msodoki :
shida mnaleta komedi kwenye maisha ya watu!!!
2026-10-07 18:13:29
2
officialmubangatz :
msisitizo tuuuuu
2026-10-07 16:35:44
2
Aniceth simoni :
uchaguzi gani hau cjaelewa
2026-10-07 18:31:59
0
lady fina :
nani kama baba mungu akutunze sana baba
2026-10-07 12:58:58
3
adamukasimil :
msisitizo tuu😁😁😁😁
2026-10-07 16:33:16
1
waziri manture :
comledia.......
2026-10-07 10:23:32
3
JHN MM🇹🇿 :
jmn kuna watu walkufa sasa mioyo inauma
2026-10-07 13:29:40
3
yohana Mpenda690 :
yote ya maslahi ya nchi yote mmeyaacha
2026-10-07 12:38:31
2
MTEKULA PHILIPO :
fact
2026-10-07 13:09:59
1
Kigogo jr :
Kuwa watu kiukweli mlizingia sana
2026-10-07 17:40:52
1
Ndenzako komesha👏 :
daa, mm nakuelewea sana
2026-10-07 12:55:00
1
Hans Ernest :
mnafanya vizur Sana lakin Sasa nyio wote mlikuwa pamoja mwanzo mpka mwisho sijui Saiv mnajadili mmepishana wapi kwa sababu wote mlishiliki uchaguz na mlikubali mshind mngefanya jitihada kuongea na yule ambae ana mawazo tofaut hii ndo italeta usawa ni ushauli tu lakini
2026-10-07 16:01:58
1
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.