@fastpromedia: Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Wilaya ya Wete, kiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara na kuimarisha usalama wa wanafunzi wanaotumia njia hizo kwenda na kurejea skuli. Ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara Kijijini hapo ya kukagua njia zinazotumiwa na wanafunzi, kwenda na kurejea skuli pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi kufuatia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa kidato cha Kwanza wa kijiji hicho alipokua njiani kurejea nyumbani akitokea skuli. #tanzania #zanzibar #fpupdates