@ukihty2: Dua Ni njia Ambayo mwanadamu hutumia kuwasiliana na Mola wake katika kuwasilisha kile anachohitaji, au kupunguziwa Madhambi yake, pia dua inaweza fanywa kwa Niaba ya mwingine yaani kuwaombea wengine Na Mola wenu Mlezi anasema: ‘Niombeni; Mimi nitakuitikieni.’ [Ghaafir 40:60]. JINSI YA KUOMBA 1 - CHUKUA UDHUU SIO LAZIMA kuwa na Udhu kabla ya kuomba du’a. Hata hivyo, kutia udhu ni njia ya kujitakasa na kuingia katika fikra sahihi kwa ajili ya kuzungumza na Mwenyezi Mungu. 2 - GEUKIA QIBLA Amesimulia Abdallah Ibn Zayd عنه رضىالله kuwa “alitoka Mtume ﷺ kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari). 3 - KUNYOOSHA MIKONO Mtume Muhammad ﷺ amesema: ‘Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya na Mkarimu. Huona haya wakati mja Wake anapoinua mikono yake Kwake (katika du’a) na kuirudisha mitupu’. [Abu Dawud] 4 - ANZA KWA KUMTUKUZA ALLAH Mtume Muhammad ﷺ amesema: “Mmoja wenu atakaposwali na akataka kuomba Dua, basi na aanze kwa kumhimidi Mola Wake na kumtukuza, kisha amswalie Mtume ﷺ Kisha anaweza kuomba chochote anachotaka’. [Tirmidhi] 5- MSWALIE MTUME ﷺ Dua ya mja haifiki kwa Allah SW hadi pale atakapo mswalia Mtume ﷺ mswalie Mtume ﷺ mara nyingi zaidi Mtume amesema: “Mmoja wenu anaposwali, na aanze kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu, kisha amswalie Mtume, kisha aombe anachotaka. [Tirmidhi]. 6 - MUOMBENI MWENYEZI MUNGU KWA SAUTI YA CHINI Abu Musa Al-Ash’ariy (r.a) amesema: ‘Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ safarini, na kila tulipokuwa tukipand mahali pa juu tulikuwa tukitamka Takbir (kwa sauti kubwa). Mtume Muhammad ﷺ akasema: “Enyi watu! Jifanyieni wema, kwani nyinyi hamumwitii kiziwi wala asiyekuwepo, bali mnamuomba Mwenye kusikia Mwenye kuona”. [Bukhari] KIUFUPI Njia bora ya kujiandaa kwa ajili ya du’a ni kufanya wudhu. kuelekea Qiblah, kuinua mikono yako , Kuanza kwa Kumsifu Allah kisha Kumswalia Mtume ﷺ na kumwomba Mola wako kwa sauti ya chini. Naomba unifollow ili wengi wapate faida kwaajili ya ALLAH ♥️
𝓕𝓵𝔂 𝓥𝓮𝓮🌸
Region: TZ
Thursday 08 October 2026 12:50:26 GMT
Music
Download
Comments
Asha wasia :
amiin[Red heart][Red heart][Red heart]
2026-10-08 18:33:00
0
Abdul Isaka Nduwarugira :
amiiiiin
2026-10-08 19:46:25
0
shazla💕 :
Amiin
2026-10-08 18:45:21
0
fifteen :
Aamin
2026-10-08 16:15:49
0
hassan t :
🥰🥰🥰
2026-10-08 13:03:14
0
jasin :
AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN
2026-10-08 18:57:58
0
To see more videos from user @ukihty2, please go to the Tikwm
homepage.