@mkakamweus2: Bella Urassa, ambaye ni dada wa marehemu Jenifer (Jeni) Urassa amesema hawezi kusema uongo, ni kweli mdogo wake alimweleza siku chache kabla ya kuuawa kuwa alikuwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yake, akihusisha hofu hiyo na mgogoro wa umiliki wa nyumba yao iliyopo Bunju, Dar es Salaam. Hii ni baada ya Jane kubadilisha umiliki (hati) ya nyumba na kusoma jina lake na jina la watoto wake kinyume na matakwa ya mumewe Laurent Kweka ambaye kimsingi ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo. Nisiwe muongo, ni kweli Jeni alinieleza kuwa ni kweli ameshughulikia hati na hati ya nyumba hiyo imetoka ikiwa na majina ya watoto wao wanne, na jina lake yeye akiwa msimamizi wao, jambo ambalo alidai lilipingwa na mume wake aliyekuwa akitaka hati hiyo iandikwe kwa majina ya wanandoa hao wawili. Jeni kwa sababu zake binafsi hakutaka kabisa hati za umiliki wa mali ikiwemo nyumba hiyo yenye thamani ya inayopindukia milioni 350 viwe na jina la mumewe. Kwa mujibu wa Bella, baada ya hati hiyo kutoka, Jeni aliwahi kusema anaamini mume wake angeweza kumuua kutokana na kitendo alichofanya cha kubadili hati hiyo ya nyumba bila idhini ya mumewe Aidha Jeni alienda mbali zaidi akachukua mkopo bila ridhaa ya mume wake ba bila kumjulisha. Hata hivyo Mkopo alishindwa kurejesha, na walivyo mtafuta mume wake aka wajibu yeye hana pesa hivyo washughulike na aliyechukua mkopo. Jeni, mzaliwa wa Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, aliuawa kwa kupigwa risasi na mume wake alfajiri ya Alhamisi, Oktoba Mosi, 2026, nyumbani kwao Bunju, baada ya kutokea kwa tafrani ndani ya chumba walichokuwa wakiishi. Akizungumzia mazishi, baba mdogo wa marehemu, Joseph Urassa, amesema familia ya kwao imeamua kumzika Jeni nyumbani kwao, kama alivyokuwa ameomba kuwa siku akifa asizikwe nyumbani kwa mume wake... Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ukoo wa familia alikoolewa, Mchungaji Tumsifu Kweka, amesema familia yao haitalumbana na familia ya Urassa na itaheshimu taratibu zitakazokubalika kuhusu mahali marehemu atakapozikwa. NOTE: 1. Ni kweli 100% kuwa Jane alifanya hila na njama za kubadili umiliki wa mali ya mumewe kwa nia ovu ya kumdhulumu. Na hata Jane alijua si halali ndio maana alikuwa na hofu kuwa mwanaume asingechukulia poa huo upumbavu. 2. Ni kweli 100% kuwa familia ya Jane ilikuwa ina taarifa zote za nia ovu ya Jane ya kutaka kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba lakini hawakumkemea wala kumshauri aache hiyo tamaa. 3. Ni kweli 100% kuwa Jane alishajipanga si tu kuachana na mumewe bali pia kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba ndio maana alishawataarifu ndugu zake mapema kuwa hata akifa asiende kuzikwa nyumbani kwao mumewe. 4. Unawezaje kumtetea Jane kuwa hakupanga kumdhulumu mune wake mali na huenda hata alikuwa katika mipango ya kumuua mumewe ni vile tu amewahiwa. Kwa nini ahakikishe katika hati hiyo hakuna jina la mume wake? Si ni kwa sababu alijua mume wake atapoteza maisha siju za karibuni iwe kwa saratani au kuuawa? Mwenyekiti mnanipa wakati mgumu sana kuwatetea ninyi wanawake. Punguzeni tamaa! Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, nayo dhambi ikiishakukomaa huzaa mauti. Si Jane tu alikuwa na tamaa bali hata ndugu zake walikuwa na tamaa ndio maana licha ya kuwa na taarifa za Jane kumdhulumu mume wake hawakumzuia wala kumshauri aachane na mpango huo hatari. Matokeo yake wamepokea maiti.#creatorsearchinsights #creatorsearchinsights #creatorsearchinsights #creatorsearchinsights #creatorsearchinsights

mkakamweusi2
mkakamweusi2
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 08 October 2026 13:58:59 GMT
280155
4600
380
260

Music

Download

Comments

neema.assey8
lovely one :
ukiwa n watoto ndio utaona Jane hakuwa n kosa lolote.Ni bora alikumbuka watoto kuliko ingekuja kugombaniwa n watu wengine watoto wakahangaika.....Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi🙏
2026-10-08 16:49:19
153
mama2son
DARE COLLECTION TZ :
Naamini kitu kimoja mpk mwanamke anaamua kubadili hati majin na asiwek la mumewe Lazim kuwe n SABABU KUU MUHIM. 1. km mume alkuw na saratan bhc mke aliamua alinde mali dhidi yke n watoto maan ikitokea mume hayupo dunian wasitesek, maan ndugu wa mume kwa Tamaa z mali ndyo sifa zao. 2. Either mke alion mume ana mambo meng y wanawek nje au watoto wa nje hvyo alifny kulind mali dhid yke na watoto wake.. NB..YOTE KWA YOTE MALI NA THAMANI ZINATAFUTWA LAKIN UHAI HAUJIRUDII JAMAN, TUFIKILIE WATOTO, WAZAZ WETU, NA JAMAA ZETU , KUWA MWEPESI KUANZA UPYA AHSANTE
2026-10-08 16:15:45
50
brown.osiah
Brown Osiah :
mimi nilishakataa mali yangu zisiandikwe kwa jina la watoto wakatafute vyao kama tukifa wote sawa ila kama nikitangulia mali itabaki ya mke sio watoto, wao wanachonidai ni elimu na chakula mpaka watakapofikia kujitegemea
2026-10-09 06:38:29
72
user8705283290424
lihaki :
mimi yote kwa yote nailaumu serikali ndio inayosababisha yote haya mpaka yanatokea mauaji kila kukicha kuhusu hati miliki hivi inakuaje mtu anakuja kubalisha majina ya hati bila kumuuliza au kumuhoji kama wako wawili au kwanini siku inabadilishwa hati msiwaite mume na mke wawepo pamoja au ndio rushwa mtu akija tu na fedha kidogo anapewa haki sasa watazikwa wengi watendaji katika sekta za serikali hasa ardhi muwe makini sana
2026-10-08 19:33:41
85
therealrakisa_tz9
🎀🌸marsha🌹🥰🥹 :
me nafikilia alitaka haki ya watoto wake
2026-10-08 18:13:45
26
ms.legal.cosmetic
Ms.Legal Cosmetic Tz :
Bado hakuna sababu ya kutoa Uhai wa mtu, uhai wa huyo dada mme wake hakua na mamlaka wa kuutoa.JUSTICE FOR JANE 💯
2026-10-09 06:45:53
18
jt.epoxy.arusha
JT Epoxy Arusha :
kwa masikitiko makubwa! Kifo cha Jane kinasikitisha kweli. Ila, je kama mume wake tayari alishatengenezewa cheti cha kifo, ndiposa cheti hicho kikatumika kubadiliki umiliki wa nyumba husika? Nashindwa kuelewa kwamba mtu unaishi naye kama mke/mume, mnalala naye chumba kimoja, kitanda kimoja, uchi wa mnyama, mwaka mzima huku yeye anajua kabisa alishakutengenezea cheti cha kifo. Je, alifanya hivyo kwa nia njema? Kwa kujiweka mwenyewe kama msimamizi wa mali na kumtoa kabisa baba wa watoto wake hao wanne, moja kwa moja huyo baba alishaondolewa kwenye ulimwengu wa walio hai na kwenye nafasi yake ya ubaba. Hamna mwenye kustahili kufa (uhai na vifo vyote vya Mungu) ila dada zetu mnafanya maisha kuwa magumu sana bila sababu ya msingi. Dah! Nasikitika sana
2026-10-08 21:57:25
10
marriott02
Duke of Edinburgh :
Nimesikia mara kibao story hiyo, marehemu roho ya marehemu iendelee kuteseka kwa tamaa zake, kawapa ukiwa watoto bure. Eeh Mungu baba wa mbinguni tuma malaika wako wa haki wakamtetee kaka wa watu mahakamani ili arudi kuwafariji wanae
2026-10-08 19:10:12
9
bensonndaki6
NDAKI jr :
mbona mm ba mke wangu tume andikisha watoto kwenye hati za viwanja, kwani kuna shida gani?
2026-10-09 03:58:16
5
user81193951412923
Stephen :
kwann abadilishe hati kwann? whay
2026-10-08 16:47:52
13
azizaa155
Azizah hasheem2 🇹🇿 :
: Wadada muda mwengine tuwe na huruma aisee hao ni wao ni watu, unabadilisha alikwambia halei wanae? Bwana kapata hasira kamuua/ tupunguzeni tamaa khaa, hao ni WATu kama sisi
2026-10-08 18:36:29
24
mama.boyd7
mama boys :
Mkishazaa mtamuelewa jane alimaanisha nini,
2026-10-09 07:39:12
5
dottosmartstore
dottosmartstore :
Maswali ni mengi 🥹Ila Jane alijua mmmewe atatangulia kufa coz alikua na kansa ona sasa yeye ndo kaanza maskini
2026-10-08 17:58:37
7
savelaemanuellugalo
savela lugalo😜 :
so kwer inavy semekan kiwanja walich Jenga kilikuwa Cha Jane ila nyumba walishilikian wote kujenga baada ya hap mmew alitak hat ya nyumbn iandikwe Kwa jina lake. ndo Jane akawa anaping akaamua hat iandikwe Kwa Majin ya watoto wao mungu aipumzsh loho yake mahali pem Amina😭😭
2026-10-09 09:52:09
8
user7173472561032
Renee :
akili kubwa mama wa kambo alinibuluza mahakama kuu tanzania pumzika baba yangu pumzika bintiyako napambana naimani nitafika
2026-10-08 17:01:55
7
h2sh17m
h2sh17m :
Congratulation Mr.Kweka
2026-10-09 03:59:48
6
user7914828524458
mrs chidy :
laurent aachwe huru
2026-10-08 18:28:02
7
tinnoh_72
TINNOH_72 :
Uwa kabisa Tamaa ya pesa bila kuitafuta ni wizi 🔥 kapewa haki yake
2026-10-09 04:14:12
5
anna.mimis
AnnMimis :
Free laurent
2026-10-08 17:57:16
10
ukhty.zuuh.saidi
Ukhty Zuuh Saidi :
ila sisi wanawake mmh
2026-10-08 17:44:34
5
julith207
julith :
tamaa mbaya vitu vyote tunaviacha hapa duniani mimi namshukulu mme wangu hunishilikisha kila kitu
2026-10-08 16:14:30
6
sekela826
MNYAKYUSA OG :
UKISHAKUWA NA WATOTO NDIO UTAJUA KAMA JANE ALIKUA NA TAMAA AU LAH!!! 😭😭😭 ..PUMZIKA KWA AMANI JANE
2026-10-09 13:50:19
4
elisianajonathan2
Elisia :
all in all haikuwa sababu kumuuwa dadangu mmachame mwenzangu hakustahili hukumu kubwa hivi pumzika kwa amani jane
2026-10-09 12:16:16
1
medicalclinic06
Danny Pio :
Kwani kabila gani hao majamaa?
2026-10-09 04:56:39
1
noka23kitchen
Dafroza Walter Nditi :
Hiyo nyumba ni ya namna gani kwanza niulizee
2026-10-09 12:21:18
2
To see more videos from user @mkakamweus2, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About