@user1392443859324: *AKILI YA KIUNGU* 📢Akili ni uwezo wa kipekee wa kisaikolojia unaomsaidia Mwanadamu kufikri,Kuelewa,Kujifunza,Kupanga na kutatua changamoto. 1 Wakorintho 10:15 [15]Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 💥Mtu mwenye akili kuna namna anavyofikri kuyaendea Mambo. Waamuzi 5:29 [29]Mabibi yake wenye akili wakamjibu, Naam, alijipa nafsi yake jawabu. 📢Akili ni ufahamu ukiomo katika ubongo wa mwanadamu unaomsaidia kutofautisha Mambo. 📢Akili ni uwezo wa kupata ufahamu ujuzi na kutambua mambo(Ayubu39:17)Daniel9:22) 📢Akili ni mtaji mkubwa kuliko/ Kabla ya vingine pesa n.k. 📢Akili ni mtaji aliopewa mwanadamu ili kuyaongoza Maisha yake Duniani kwa ufanisi. Kumbukumbu la Torati 1:13 [13]Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. *AINA ZA AKILI* 💥Akili ya kuzaliwa Hii ni akili ambayo kila mtu anayo(Mwanzo 2;7) 💥Akili ya Darasani. Ni akili ya kusoma na kufundishwa darasani. 💥Akili ya Maisha Hii ni akili unakuta mtu hajasoma lakini anamatokeo makubwa ya kimaisha. 💥Akili ya Kiungu. Ni akili ambayo mtu hazaliwi nayo hasomei darasani, Bali ni Mungu anamuingizia mtu anayeitaka na kuitafta kwake. Ni sehemu ya akili ya Mungu anayompa mtu kwa ajili ya kutimiza kusudi maalumu. 2 Timotheo 2:7 [7]Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. *Umebarikiwa*🙏 Ndimi Moses Selya Masanja 0785475703 08/10/2026.

Moses
Moses
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 08 October 2026 17:07:22 GMT
113
8
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @user1392443859324, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About