@millardayo_: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza mpango wa kuondoa matumizi ya kadi za kukwangua za muda wa maongezi ya simu na kuhamia katika mfumo wa kidijitali wa kuongeza salio, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhamasisha uchumi usiotumia fedha taslimu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TCRA, zoezi la majaribio la kusitisha matumizi ya kadi hizo litaanza Januari 1, 2027, huku shughuli za uhamasishaji kwa umma zikiwa zimeanza Oktoba 1, 2026. Zoezi hilo litafanyika katika mikoa mitano, ambapo Dar es salaam litahusisha Wilaya zote, Dodoma litahusisha Jiji la Dodoma, Chamwino, Kondoa Mjini na Kongwa, huku Arusha likihusisha Jiji la Arusha, Wilaya ya Arusha, Meru na Karatu. Kwa upande wa Mwanza, zoezi litahusisha Nyamagana, Ilemela na Misungwi, wakati Mkoa wa Mbeya litafanyika katika Jiji la Mbeya, Wilaya ya Mbeya na Mbarali. TCRA imesema mpango huo unalenga kuongeza matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali, kurahisisha ununuzi wa muda wa maongezi pamoja na kupunguza uzalishaji, usambazaji na utupaji wa kadi za kukwangua ambazo zina athari kwa mazingira. #Millard AyoUPDATES
millardayo
Region: TZ
Thursday 08 October 2026 18:01:25 GMT
Music
Download
Comments
Pearl pink :
hatimae na sisi tutakua tunasema enzi zetu tulikua tunakwanguaga vocha
2026-10-08 18:41:25
224
Abdallah :
Halafu ziwe za kuosha au tufahamishe uzuri
2026-10-08 18:06:13
74
Africana fans :
MARA ya Mwisho ckumbuki Lini kuweka vocha
2026-10-08 18:30:56
40
Monicah🇹🇿🩶 :
Hatimae wanangu namm watakuja kuniona mhenga nitawambia enzi zetu kulikuwaga na vocha za kukwangua 😂😂😂😂
2026-10-08 18:49:34
38
Yaredi mtokambali28 :
step by step the coming of ??? some one help me🙏
2026-10-08 20:05:31
0
@cute :
tunaletewa za ku scan au
2026-10-08 18:33:18
17
NASH..62🦋⚽️ :
Kwaiyo zitakuja za kupulizaaa Mashallah 😂😂
2026-10-08 18:43:59
8
stevelee :
sawa lakn tukiunga bado la wiki litumike wiki husika ety🔥🔥🔥
2026-10-08 18:37:34
12
Mrs haydar :
Heeee mbn me nime ach tok mwak juz kumb bd zipo
2026-10-08 20:54:43
0
🌚🌚 :
Mmmmmh
2026-10-08 19:50:23
0
D A B Z I E 🇿🇲🇹🇿 :
Zambia washamalizana na scratch cards toka last year
2026-10-08 20:04:39
0
Baby Girl💗 :
Kwn Kuna Mtanzania Ambaye Bdo Anatumia Hzo💔😂
2026-10-08 19:20:36
4
💮Milly💮 :
wengine hatujui namba ya sili
2026-10-08 18:48:16
5
Mr anything :
munaleta za bloototh connect
2026-10-08 18:35:20
0
jullove23 :
Mimi hamna habari naziaminigi Kama hizi taarifa zinazotolewaga na kaka millardayo yaani ivi taarifa ikishatolewa na kaka Milla ndo naaiamini sijui kwanini
2026-10-08 18:21:55
13
🐾 :
Asante studio😭😂
2026-10-08 18:38:48
5
Bees Quan. :
SONGESHA.
2026-10-08 20:48:02
0
🤏𝓓𝓲𝔃𝔃𝓸𝓴𝓱𝓪𝓷🇹🇿 :
Sasa tukitaka kukopa nipige tafu tunalupajeee😀
2026-10-08 18:30:21
9
Prime_niccoh💚🩷 :
January 🤦🏻♂️mbali kwel si wangesem ata november ningeenda kuzikusanya kwa mangi😢
2026-10-08 19:20:12
2
DidY🗣️……. :
Kuwepo na WIFI ya Taifa😂Na hiyo WIFI iwekwe kwenye Bajet ya mwaka😂Asante Mh. Millard Ayo nishushe😂
2026-10-08 20:26:57
1
Nature🏞️🌿 :
tuletewe za kupaka
2026-10-08 18:57:34
0
@Kipepeo🦋 G :
Sasa vipi mama yangu sasa atafanyeje huko 🥺
2026-10-08 19:39:20
0
munisi :
watuletee za kubondaa tuu
2026-10-08 18:31:52
2
voisaclassic92 :
tutafika tu huko sio muda maake shetani ameshapanga kila kitu kwamba hakuna kuuza wala kununua kwa cash inakua mwendo wa namba tu
2026-10-08 19:18:37
2
Leahmussa :
saw sijakata na shangazi yangu nitamtumia je sasa huku songesh wananidai Ata nikiwa nmelala usiku
2026-10-08 18:51:14
2
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm
homepage.