@uhondo.tv: Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Shukrani Amosi, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mumewe katika Mtaa wa Mkwajuni, Kata ya Kiwanja cha Ndege, mkoani Dodoma, usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na shemeji wa marehemu, mwanaume huyo anadaiwa kumchoma mkewe kisu shingoni, kisha kuondoka nyumbani na kwenda kunywa pombe. Baada ya kurejea, mwanaume huyo anadaiwa kumwingilia kimwili marehemu akiwa tayari amefariki dunia. Taarifa zinaeleza kuwa mtuhumiwa alijisalimisha katika kituo cha polisi kulipopambazuka, huku mazingira ya tukio hilo yakiendelea kuibua maswali kuhusu kilichotokea kabla na baada ya mauaji hayo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkwajuni, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Maxmilan Jeremia, amesema kuwa wivu wa kimapenzi ndio unaotajwa kuwa chanzo cha tukio hilo hadi sasa, ingawa chanzo hicho hakijathibitishwa rasmi na vyombo vya uchunguzi. Akieleza namna alivyopata taarifa za tukio hilo, Maxmilan amesema alipigiwa simu na wananchi saa 8:06 mchana na kupewa taarifa kuhusu tukio hilo, ndipo walipoelekea eneo la tukio kwa ajili ya kufahamu kilichotokea. Amesema walipofika eneo hilo, walikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala kifudifudi, ukiwa na jeraha kubwa katika eneo la shingo. Kwa mujibu wa maelezo ya awali yaliyotolewa na shemeji wa marehemu, pombe pia imetajwa katika maelezo ya tukio hilo, baada ya mtuhumiwa kudaiwa kuondoka kwenda kunywa pombe kufuatia kumchoma kisu mkewe. Hata hivyo, bado haijafahamika rasmi kilichosababisha mauaji hayo, huku uchunguzi wa vyombo husika ukitarajiwa kubaini mazingira kamili ya tukio hilo na hatua zaidi za kisheria dhidi ya mtuhumiwa. #UhondoTVUPDATES

Uhondo TV
Uhondo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 09 October 2026 16:52:52 GMT
146256
4343
260
474

Music

Download

Comments

babydiary02
baby diary❤💘❤ :
af leo hii mtu analilia kuolewa
2026-10-09 17:56:45
118
nuskam29
Nuskam :
Saiv nikiona wanandoa wanagombana nawa report 🥺
2026-10-09 18:45:54
36
shuuhatun3
Shuu hatun ❤️🦋 :
Alikuwa anamnyima unyumba mmewe
2026-10-09 18:01:18
17
babydrama01_
nujrat😜 :
ctak kuolewa wala ctak mahusiano 🥺
2026-10-09 18:27:31
27
wahyder5
❤️wahyder❤️ :
Yaan mtu akikutongoza unaanza kujiuliza huyu ndo ataeniua nn
2026-10-09 18:54:08
24
charitymtui2
cheryl🪽 :
nobody is safe from the hands of men💔
2026-10-09 18:47:56
1
mafiaislandfinest
mrs engineer og🦋🌹🌹 :
dodoma na arusha mama mmoja baba mmoja🙌🙌🙏🤲🫴mwenyezmungu isaidie hii mikoa
2026-10-09 18:19:29
15
russian_wrld
R U S S I A N 🎲 :
Inamaana Kila Mtu Kauona Utupu Wangu?
2026-10-09 18:58:27
4
melisiana79
Melisiana :
ivi mi mauliza kwani kuolew ni lazima ?
2026-10-09 20:27:35
1
user3767062461926
Radhia ally :
naona kama mm ndo yanaenda kunikuta maana mwanaume simuelewi kabisa
2026-10-09 19:09:45
7
rehemaabdallah33
Rehema :
Jaman mtatumaliza 🥺
2026-10-09 18:07:55
7
rayaww.tiktok.com2
ℝ𝔸𝕀𝕐𝔼★╠♥︎ :
Itabidi nimuambia huyu bwana Nimeghairi kuolewa Nianze kuelekea gulf
2026-10-09 18:26:14
9
kaaaaaa123413
Dahuaaa1234 :
Alikua amnyima nini
2026-10-09 17:57:45
2
sugardhdhhjjdjdj
edinho30 :
asa mtu hatak kutoa haki yake afanyeje😁
2026-10-09 20:03:35
0
jescaantony4
Narony💕 :
Yaani watu wanavyoilaumu ndoa,Mimi dada yangu aliuliwa na boyfriend wake sio mume Yaani mpenzi tu,kwaiyo musiseme ndoa semeni mahusiano ni mabaya
2026-10-09 18:56:26
5
nyokamdada
NyOK@md@d@ :
pumzikeni kuolewa jaman eee mimi nipo mwenywe mwaka wa 3 huu mbna naishi
2026-10-09 20:03:51
0
kuchile775
bts army 💜 :
Kila nikiona matukio kama haya moyo wangu unaona kama ndoa ni uwanja wa vita
2026-10-09 18:45:48
2
mom.giovearn
lulu john☑️ :
😁😁😁mm nakipgo hpn
2026-10-09 19:51:22
1
nyanumbu7
minah juma :
mhh jmn alafu nibwa dodoma km wa kwangu mie mpk naogopa mana ana wivu mpk anakera ugomv mkubwa simu yng iktumika bc nmepgiwa na mwanaume na anasema ipo.siku nkchoka kuongea utajua ujui yan nataman ata nimtoroke
2026-10-09 19:46:23
0
baby.zyder
Miss🌸 Zyder💜💋 :
Daah mbn saiv matukio ya vifo vya mauaji ni vingi ad tunaogop daah Allah atujalie mwisho mwema
2026-10-09 19:50:46
1
nady_naah7
nadya💋💋💋 :
mwanamke alikuwa anamnyima unyumba mwanaume au ni vipi
2026-10-09 18:26:00
2
unlimited.money12
Unlimited money :
sisi wa Arusha tumetulia sasa semeni na apo
2026-10-09 19:16:18
3
arafahz3
mama princesses 🥰😍 :
jmn wanawake tunauliwa sana🥺🥺
2026-10-09 18:54:59
2
myp028
PAULINDA🥰🔐🙏 :
Ndoa🙌🏿🙌🏿
2026-10-09 18:31:21
2
user5131105499631
Bethina :
Wanandoa wanandoa wanandoa nimewaitax3
2026-10-09 18:12:08
3
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About