@papaa.marsha1: WERRASON ANAKUAMBIA HATOKI NA MWANAMUZIKI NYUMBANI Balozi wa Amani Le Roi De La Foret Noel Ngiama Makanda Werrason hivi karibuni alikua mji wa Muanda huko Congo katika aonyesho lake la Tar 26 Sep 2026 Muanda ni mji uliopo pwani ya Bahari ya Atlantiki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwenye mdomo wa Mto Kongo eneo hili linapatikana katika Mkoa wa Kongo ya Kati Wakati wa Onyesho likiendelea ambalo lilipokelewa na Umati mkubwa sana wa watu mashabiki kuna namna walikua wakipaza sauti kana kwamba wanataka kusema kitu Werrason alisimamisha Muziki na kuwauliza mnasemaje basi sauti za wengi zilimuelekeza Werrason kwamba Kuna kijana katika mji huo analijua vema Gitaa la solo Werrason husifika sana kupendwa na watu wa hali ya chini na vijana aliwasikiliza mashabik wake na kumuita kijana huyo Stejini Kijana alipanda na Werra aliwaomba wanamuziki wake na Kiongozi wa Band Papy Kakol wampe nafasi kijana huyo wasikie kipaji chake Kijana aliulizwa na Werra utupiga nini Kijana akasema yeye amkekulia katika upigaji gitaa na vitu anavyo vipenda ni muziki wake Werrason wa Wenge Musica Maison Mere hivo atapiga vitu vya Wenge kijana hakuishia hapo akashukuru kwa kupata nafasi kupanda jukwaa hilo na kukutana na mtu wa ndoto yake katika muziki wake Werrason akampa nafasi na kabla hajaanza kupiga Werra alisema Mimi huwa sitoki na mwanamuziki nyumbani au ndugu yangu bali mashabik ndio huwa wanachagua mwanamuziki wa kuungana nami hivo ukifanya vibaya watakukataa ukifanya vizuri watakupokea Werrason huchukua vijana wa kuungana nao kwa kuwafanyia test mbele ya mashabik wake wakikupitisha basi ndio unajiunga kundini Kijana huyo alilikung'uta gitaa kweli kweli na kupiga nyimbo nyingi za Wenge kwa ufasaha hasa sebene na Werrason na mashabiki wakakubali Werrason akamuita kiongozi wa band Mpiga Drum Papy Kakol na kumuuliza unasemaje tuondoke na Dogo Kakol akajibu kwamba kijana nilikutana nae kabla ya onyesho na tulizungumza na kijana huyo alimpigia gitaa Kakol na kufurahishwa nae na kumueleza wewe ni mpiga gita hodar jion njoo kwenye show ukipata nafasi uonyeshe uwezo wako Hivo kakol na Werra waliridhia kumchukua kijana huyo na Werra akamuambia kafunge Mizigo yako tunatondoka wote kuelekea Kinshasa hapo ndipo Werrason Kamfungulia Dunia kijana huyo ili awe anacho kitaka kama vile msemo wa Clouds unavo sema Clouds ambao wana jukumu la Kumshusha Werrason Dar es Salaam Tanzania Pale Super Dome Masaki Nov 6 2026 Dacota de lavida 10 Oct 2026
@R.M.B. Cocktails🍹🍸🥤:km kuna kitu Werason anaupiga mwing bas kuamin vipaj vya mitaan. kawatoa weng. kuanzia kapaya, kimbangu, sarah solo, Afredo na uyu. na dogo mmoja iv naskia amefark. Mungu ambarik sana
2026-10-20 11:37:08
2
James kibosho :
ngiama ndio style yake iyo kijana wengi hua anawachukua kwenye stage wakishakubalika na,mashabiki 🤣
2026-10-23 08:50:29
2
Ritha Thadeous :
best of the best
2026-10-11 02:18:36
3
Mkali semwanza :
hatari sana✌
2026-10-20 11:38:00
1
004 :
%100
2026-10-11 11:42:49
2
charlzchito :
Alaa!! kumbe " matondi makasi "Ndeko dacota " opesi ngai Sango nalingaki😁, Ni kweli Werra usajili wake unatoka kwa Wanajamii ( ndomaana juzi nimeona kipande cha Show nkamuona huyu dogo , Yaani hpo Sifa uwe na program nzima ya Mshua..Kwhyo Alfred katulia tu pembeni naye ana miezi michache tu kundini😃😄
2026-10-10 11:07:58
1
shimma_decor lights :
aiseee hii kubwa kuliko eeh keba keeba keeeba😜
2026-11-05 19:55:12
0
Mzozo 😷 :
[Fire]
2026-10-20 10:56:06
1
mckevy :
🔥🔥🔥
2026-10-12 00:32:20
0
Man :
😁😁😁
2026-11-05 16:31:43
0
To see more videos from user @papaa.marsha1, please go to the Tikwm
homepage.