@khamissaleh06: #creatorsearchinsights #createsightinsight 🇫🇷 Msichana mmoja Mfaransa Muislamu amezua mjadala mkubwa baada ya kutoa kauli ya ujasiri akiwa katika moja ya studio za televisheni kuhusu suala la hijabu. Alisema kuwa mamlaka zinapambana na hijabu ili kuficha kushindwa kwao kisiasa katika kutatua matatizo halisi yanayoikabili jamii, kama vile ukosefu wa ajira, kupanda kwa gharama za maisha na masuala ya usalama. Alisisitiza kuwa hijabu yake haimdhuru mtu yeyote, wala haimzuii mwanamke kufanya vizuri katika masomo au kufanya kazi katika taaluma mbalimbali, ikiwemo udaktari na ualimu. Alieleza kwamba kwake, hijabu ni uhuru wa mtu binafsi na imani ya kidini, hivyo haipaswi kutumiwa kama kisingizio cha kukwepa kujadili matatizo halisi yanayoikabili jamii. Kwa ujasiri, alihoji: Ni sababu gani zilizofichika zinazofanya kipande hiki cha kitambaa kiwasumbue baadhi ya taasisi na wanasiasa nchini Ufaransa? Kauli yake imeibua mjadala mpana katika jamii kuhusu swali moja muhimu: Je, hijabu ni tatizo la kweli, au imegeuzwa kuwa suala la kisiasa ili kuficha kushindwa kushughulikia matatizo halisi? #SufianMzimbiri
Khamis Saleh
Region: TZ
Saturday 10 October 2026 15:56:22 GMT
Music
Download
Comments
Dee smile :
Allah a
2026-10-11 03:53:53
0
⭐maham'sly♉ :
khaallassss....
2026-10-11 03:43:50
0
Harsher camal! :
💯 Allah akbar
2026-10-10 22:16:33
1
user17531367682971 :
Allah Akbar
2026-10-11 04:30:12
0
chakachaka :
🤲🤲🤲
2026-10-11 13:39:06
1
To see more videos from user @khamissaleh06, please go to the Tikwm
homepage.