@jambotv_: VIDEO: Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewachekesha Watanzania wanaoishi Uingereza baada ya kutania kuwa ushindi wa Simba dhidi ya Yanga ni tukio kubwa linalostahili kujadiliwa hata nchini humo. Amesimulia kisa cha mtoto aliyesoma sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita bila kushuhudia Simba ikiifunga Yanga, huku akitaja pia mtoto wa rafiki yake aliyeshangaa kusikia Simba imeshinda na kuuliza kama timu hiyo inaruhusiwa kuifunga Yanga! Dkt. Mwigulu ametoa utani huo jijini London, Uingereza, wakati akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini humo katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji la Diaspora la Tanzania (Tanzania Diaspora Business & Investment Forum 2026). Credit: @tbc_online