@uhondo.tv: Mwili wa Michael Andrea, mmoja wa askari Polisi waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Oktoba 8, 2026, eneo la Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, umeagwa nyumbani kwao katika Mtaa wa Railway, jijini Dodoma, kabla ya kuzikwa kwa heshima za kijeshi na kidini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimetawaliwa na majonzi na simanzi, huku wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa familia wakishindwa kuficha huzuni kufuatia kifo cha askari huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 24. Katika sehemu ya mazishi hayo, risasi tano zilipigwa hewani ikiwa ni sehemu ya taratibu za heshima za kijeshi kwa marehemu. Michael Andrea amezikwa katika Makaburi ya Kilimo Kwanza jijini Dodoma, huku mazishi yake yakihitimisha safari ya maisha ya askari huyo aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ya kusikitisha. #UhondoTVUPDATES

Uhondo TV
Uhondo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 12 October 2026 18:46:10 GMT
15933
367
11
25

Music

Download

Comments

its.ferion
its ferion :
Kijana kaondoka mdogo sanaa
2026-10-12 19:53:06
2
wilbertkwiligwa
Wilbert Kwiligwa :
mungu akupunguzie adhabu ya kabuli
2026-10-13 10:43:14
0
onesmomayengo
Onesmo mayengo :
pumnzika kwa aman kaka
2026-10-13 12:56:07
0
j.linny0
@J Linny🥰🥰 :
pumzika kwa amani michael
2026-10-13 03:59:33
0
userrcn8ultzoc
hadija bakary :
mungu ampunguzie azabu ya kabuli[Hands open][Hands open]
2026-10-12 20:28:59
0
user7066667795308
Queen 👑 Dianna ❤️ :
poleni familia mungu awatie nguvuu
2026-10-12 21:24:00
0
samsonkazimoto
Samson Kazimoto :
pole sana kwa familia niliona mama yake nikashindwa kujizuia😭😭
2026-10-13 07:17:42
0
mkanjeg
gmm :
pumzik kwa aman
2026-10-12 20:46:30
0
ndembo591
S@NKARA T :
p1
2026-10-12 19:31:30
0
haland6224
haland :
🤲🤲🤲
2026-10-12 18:51:55
0
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About