@kiswahilitvonline: Hizi ni kumbukumbu za bendi ya Westlife kikundi ambacho kilitikisa kuanzia miaka ya 90 lakini jinsi miaka inavyozidi kwenda idadi yao ya watu 5 inaendelea kusambaratika hatua kwa hatua. Hata hivyo hivi karibuni kuanzia Oktoba 22–26, 2026 watafanya ziara yao kubwa ya maadhimisho ya maadhimisho ya miaka 25 inayokwenda kwa jina la Westlife 25:The Anniversary World Tour ambapo watatumbuiza wajumbe watatu tu ( Shane Filan, Nicky Byrne, na Kian Egan). Wajumbe wengine wawili hawata kuwepo kwasababu mmoja ambaye ni Mark Feehily, bado ni mwanachama lakini anamatatizo makubwa ya kiafya hivyo ameingia kwenye mapumziko ya lazima ya kutotumbuiza jukwaani. Mwingine ambaye ni Brian McFadden, alishajiondoa kwenye bendi hio tangu mwaka 2004 na akaendelea na miradi yake binafsi ya kimuziki.