@itslinangwa: Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza imemhukumu Suzana Marwa, maarufu kama Maswi (78), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kukutwa na bangi yenye uzito wa kilogramu 33.25. Suzana alikamatwa Machi 29, 2026 katika eneo la Bugarika Kaskazini, baada ya Maafisa wa DCEA kufanya upekuzi nyumbani kwake na kukamata bangi iliyokuwa kwenye mifuko miwili na ndoo ya plastiki. Katika hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi Clement Tuji alieleza kuwa umri mkubwa wa Suzana ungestahili kuzingatiwa katika kumpunguzia adhabu, lakini Sheria inaweka kifungo cha lazima cha miaka 30. Mahakama pia iliamuru bangi hiyo iteketezwe na fedha taslimu shilingi 195,000 zilizokamatwa zitaifishwe. #pppppppppy #viral
Nastofficialy
Region: TZ
Tuesday 13 October 2026 05:10:56 GMT
Music
Download
Comments
Nusuraty :
jamn mbn mzee san jamn
2026-10-13 10:40:08
0
Suzan Laurence :
Suzana tena
2026-10-13 13:18:15
0
g'father :
mabilion yanaibwa Kila siku hakuna anae kamatwa wala kurudisha fedha lakini angalia masikini wanavyo kamatwa sasa
2026-10-13 08:27:42
24
Ngoreme princess :
miaka 78+30= 108.
Hapa kula juu ya Jela, ugonjwa juu ya Jela, Jeneza juu ya Jela😭😭😭😭
2026-10-13 08:42:16
19
user1191510961429 :
afu mbona mi nipo bugarika ila sijuhi kinachoendelea huku 🥺🥺🥺
2026-10-13 11:20:28
2
Catherin fashion Dizain totoz :
MUNGU aileze lohoyake mahali pema peponi amina pole Suzana. na iwefunzo Kwa wote
2026-10-13 07:07:34
13
nuriath kakuru :
mmhh jaman nimejisikia vibaya sana,mama huyu ni maisha tu magumu jaman mungu tusaidie walinde mama zetu mungu akusaidie bibi angu🥹🥹
2026-10-13 07:09:21
16
Justa :
masikini dah mpaka najikuta kuliaaa, Nan kama mam
2026-10-13 16:19:50
1
ester Joseph :
mama etu jamani 😭😭
2026-10-13 08:13:21
2
minah@❤️❤️✌️ :
sas jamn mbn anafia jera wangemuacha tu
2026-10-13 07:50:08
2
Hellen tedido :
yaaani wanaoua watu kila siku hawakamatwi na hawajulikani walipo why bangeeee??
2026-10-13 13:36:53
1
user9477144609281 :
inauma sana
2026-10-13 06:14:36
2
mkenytz_2007 :
jamn mtaa wangu umeshindikana daaaaah so poa
2026-10-13 19:45:56
0
Rashmii :
Mmh
2026-10-13 19:34:22
0
wantiko :
matilioni yananyakuliwa hamsemi
2026-10-13 19:32:58
0
J7 official :
inchi yetu ya ahadi, nachoka mm ngja nikae kimya
2026-10-13 18:52:55
0
Bahati Evaristo :
Dahh 😭😭😭
2026-10-13 07:18:40
1
Rughe Madevu :
Tz tuna Sheria za hovyo, mafisadi hawakatwi Wala kuchukuliwa hatua, walala hoi na wahangaikaji ndo wanamulikwa na Sheria.
2026-10-13 09:00:14
0
mag💖🥰🥰 :
jaman hiv nikwer ,,nakama nikwel mungu shusha hiyo elinino ,huruma sio malez ,,tufe wote ikibidi ,,na mungu aanze kuumba upya
2026-10-13 12:16:54
0
Thomass Wambura :
duuh
2026-10-13 17:39:14
0
bintfaustini5 :
Kama Paulo na Sila walifungwa mageleza milango ikafunguka na uyu bibi milango ikafunguliwe akawe uhuru
2026-10-13 19:46:13
0
micajunia :
wamwachie bhana maisha magumu Sana SS tuko. mtaan tunaona mbna mafsad hawakamatw
2026-10-13 17:17:56
0
🦋BUTTERFLY -GLOW🦋✨ :
Asamehewee jmn
2026-10-13 07:55:32
0
user2842790795373 :
ila basi tu 😭😭😭🙏
2026-10-13 17:45:27
0
Athuman Omar :
mbona adhabu hii nikubwa wangapi wanaiba mali za uma je hawa wamehukumiwa miaka kinagapi
2026-10-13 15:29:56
0
To see more videos from user @itslinangwa, please go to the Tikwm
homepage.