🇦 🇲 🇦 🇳 Æ🇵 :
Dizasta verse
Majuha wawili wamekaa kitako
Kwenye egemeo, wakiwa high na ma-pot use
Wanalijadili sana jina langu kila leo
Ku-prove kwamba I'm the important news
Walipo wao, ujinga upo kando wana-share
Uwezo wangu unawa-confuse
Wanakuja double wanakuta nishaji-double
Wananywea, I'm like sum of the squares of Hypotenus
Gen Z wanawacheki marapa, rappers wanacheki ma-master
Alafu ma-master wanacopy Moves
Wakiona hesabu wanadata
Ku-rap wanaacha wanatupa, kalamu chini na kuanza kufollow views
Wana-prove pesa hainunui talent, Pen rules
Mistari ka' vile curses kwenye Dead Books
Nasambaa mfano wa Airbone infection, wanahemea juu
Na-spit virus ka nime-test flu
Eyo punchlines focal
Lyrics zangu local , style yangu nyoko
Knock knock straight to the Goat Conversation
Wakati mi' Simba, na sisikii mtu akisema fyoko
Bila wings nagusa tu maanga
Kwa dondoo kama James, natupatupa nanga
Narusha tu mabanga kama Langa kafufuka, huu mzuka
mkubwa flow nasty ka' uchi una Fungus
Yeah my mommy G, and my honey Sweet
Hustle mode, cycle so small, Nigga Money big
The return of the King, Makaveli
Niki-rhyme utasema n'na-swing na machete
Wanaheshimu kazi zangu thabiti
Sidanganyi umma na namba zangu halisi
Nafanya kwa sababu, sababu zangu yabisi
Maandishi stahiki kama kalamu ya wahakiki
Nanyonga biki siju utabonga kipi?
Nipo kwenye handaki na sitoki ka' kisiki
Sifugi mabishoo, ma-fans wangu wabishi
Mi mwenyewe mbishi October sikutiki
Maisha yangu ni simple, jina symbol,
Sauti yangu inaamsha watu utasema signal
Vikao vinawekwa kuhakikisha kwamba sipo
Tatizo nimekuwa muhimu sana ku-ignore
Ukini-diss we shenzi type
Hype hii yabisi, kimiminika, gesi at the same time
Ma-deep thinker wako terrified, akaunti hii ya tenzi iko verified
Very fine, very nice
Benki kuu ya vina na flow
Ona nina rap kufa ka' nina bima ya roho
Calm under pressure, master nina control
Kwa protocal za ki-master na Dizasta ndio jina la show
Kusanya vichwa kati yenu
Fanya tafiti sasa kwenye kila kazi zenu
Majibu yote yachochee hasira ndani yenu
Kwamba shule hii haifai kwenye syllabus zenu...
2026-10-13 14:47:05