@kiswahilitvonline: Kosa kubwa tunalofanya kila siku ni kuamini kwamba tuna muda mwingi mbeleni. Tunasema "nitafanya kesho," "ntaanza wiki ijayo," au "ntabadilika mwezi ujao." Kwenye filamu ya Rocky III, Apollo Creed alimfokea Rocky maneno yaliyobadilisha maisha yake: "There is no tomorrow!" (Hakuna kesho!). Ukweli ni kwamba, kesho haijatengenezwa kwa ajili ya watu wanaosubiri, bali inatengenezwa na kile unachokifanya SASA HIVI. Acha kuahirisha malengo yako. Anza hicho unachokiogopa leo.