@madamemaryamhealth05: HAYA MAAMBUKIZI 2 NI HATARI YANAPOKUWA PAMOJA! ⚠️ Je, unajua kwamba mtu anaweza kuwa na maambukizi ya HIV na homa ya ini kwa wakati mmoja? Maambukizi haya yanapokuwa pamoja, yanaweza kuongeza changamoto katika utunzaji wa afya, hasa ikiwa ini limeathirika au matibabu hayafuatwi vizuri. Ndiyo maana ni muhimu kupima, kujua hali yako ya afya na kupata ushauri wa mtaalamu. Kwa mwenye HIV na Hepatitis B au C, daktari huchagua matibabu kwa kuzingatia aina ya virusi, hali ya ini na dawa anazotumia. Kumbuka: Kuwa na maambukizi haya mawili si mwisho wa maisha. Kwa uchunguzi, matibabu sahihi na ufuatiliaji wa kitaalamu, mtu anaweza kutunza afya yake vizuri. #lishebora #hepatitis #afya #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪
Madam Maryam health
Region: TZ
Wednesday 14 October 2026 08:52:09 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @madamemaryamhealth05, please go to the Tikwm
homepage.