@jamiivoice_: TARAKEA BAR YATEKETEA KWA MOTO ARUSHA, SHOTI YA UMEME CHANZO.I Moto mkubwa umezuka majira ya alfajiri katika eneo la Shamsi jijini Arusha, na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali katika sehemu ya kula chakula na vinywaji inayoitwa tarakea bar, Taarifa zinaeleza kuwa moto huo ulianza baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme kwenye transformer, na kusababisha moto kusambaa katika eneo hilo Mbali na baa hiyo, moto huo pia umeteketeza vyumba 14 vya kulala wageni, pamoja na mali mbalimbali zilizokuwemo ndani, Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mratibu mwandamizi Oswar mwanjejele ameeleza kuwa chanzo cha moto kinahusishwa na hitilafu hiyo ya umeme, iloyoanzia kwenye transfoma huku juhudi za kudhibiti na kuzima moto zikifanyika kwa takribani saa nne. Akizungumza kuhusu tukio hilo, meneja wa eneo hilo amesema hasara kubwa imejitokeza kutokana na kuteketea kwa mali mbalimbali zilizokuwa ndani ya baa na nyumba hiyo ya wageni. Amesema tukio hilo limeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za biashara zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo. Aidha, moto huo umeathiri pia ajira za wafanyakazi waliokuwa wakitegemea shughuli za eneo hilo kwa ajili ya kujipatia kipato

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 14 October 2026 11:49:50 GMT
19562
219
2
13

Music

Download

Comments

gproductions002
gproductions002 :
ya lini hii
2026-10-14 16:24:49
0
davidmassawe961
BABA IVAN&MAMA IVAN& IVAN🌹🌹❤ :
naomba aliyepost amsalimie kaka yangu aloyce Hapo kwenye duka la Tv
2026-10-14 13:52:59
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About