@rosesjtspyi: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 📢 Kwa yeyote ambaye anahitaji kazi kwa dhati na yuko tayari kupambana ili kubadilisha maisha yake, tafadhali nisome vizuri. Kuna nafasi za kazi kwa watu wenye ujuzi katika maeneo yafuatayo: 🔹 Mafundi wa gereji 🔹 Mafundi wa ujenzi 🔹 Wachoraji wa heena, piko 🔹 Wafanyakazi wa kazi za ndani SIFA ZA MWOMBAJI: ✅ Awe mtu mwenye nidhamu na heshima. ✅ Awe amejifunza dini hata kwa kiwango kidogo, na awe na nia ya kuendelea kujifunza. ✅ Apende kujistiri na kuzingatia maadili mema. ✅ Awe mchapakazi, mwenye bidii na asiye mvivu. ✅ Awe na malengo ya maisha na nia ya kujikwamua kiuchumi. ✅ Awe tayari kufuata maelekezo na kufanya kazi kwa uaminifu. TAFADHALI, NINASISITIZA JAMBO MOJA! Kama kweli unahitaji kazi, nipe nafasi ya kukusaidia. Usinifuatilie au kuniomba msaada halafu unapotea, au kufanya jambo hili kuwa usumbufu. Nafasi hizi ni kwa watu wenye nia ya kweli ya kufanya kazi, si kwa ajili ya mazoea au kupotezeana muda. Kama wewe ni mtu wa kujituma, unayejua thamani ya kazi na unayetaka kusonga mbele kimaisha, niandikie kwa nia ya kweli. Kumbuka: Mafanikio yanahitaji juhudi, nidhamu, uvumilivu na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Allah atufungulie milango ya riziki iliyo halali na atuwezeshe kusaidiana kwa nia njema. Aamiin. 🤲
marosa
Region: TZ
Thursday 15 October 2026 03:17:05 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @rosesjtspyi, please go to the Tikwm
homepage.