@imadiabeid: SMZ NA REAL MADRID KUSHIRIKIANA KUIBUA VIPAJI VYA MICHEZO ZANZIBAR Na Imadi Abeid, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ushirikiano na Real Madrid utaimarisha ukuzaji wa vipaji vya michezo Zanzibar. Akizungumza Oktoba 14, 2026, wakati wa ziara yake katika akademia za Real Madrid nchini Hispania, Dkt. Mwinyi amesema uwekezaji wa SMZ katika miundombinu ya kisasa ya michezo unahitaji kuambatana na mifumo bora ya uendeshaji na ukuzaji wa vipaji. Amesema ushirikiano huo utatoa fursa kwa makocha wa Zanzibar na Real Madrid kubadilishana ujuzi na uzoefu, pamoja na kutumia viwanja vilivyojengwa kuibua na kukuza vipaji vya vijana. Aidha, amesema akademia za Real Madrid hazijikiti katika michezo pekee, bali pia zinazingatia elimu ya darasani ili kuwaandaa vijana kwa maisha ya baadaye. Dkt. Mwinyi amewahimiza vijana wa Zanzibar kujitokeza kujiunga na akademia hizo na kushiriki mafunzo yatakayotolewa na makocha wa Real Madrid huku akieleza kuwa fursa hiyo itasaidia kukuza vipaji vyao na kuimarisha uwezo wao katika michezo.

IMADI ABEID
IMADI ABEID
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 15 October 2026 04:41:05 GMT
3334
256
6
11

Music

Download

Comments

mussa.ramadhan17
Mussa Ramadhan :
raisi ungeenda barcalona
2026-10-15 08:30:10
0
user1343232312
mo :
raisi wetu huna baya
2026-10-15 08:01:24
0
rehemamohd452
rehemamohd452 :
first nasema Rais Mwinyi anatosha kila sekta
2026-10-15 07:49:19
0
muhammed.suleman585
Muhammad Selemani👏👏 :
🫡🫡🫡
2026-10-15 05:19:34
0
mrnyomii
Mr Nyomii :
Ntu na naja enda mpira upuuzi TU vitu vyenyu umuhim zaidi mmeziacha
2026-10-15 08:06:39
0
mamy.luu50
mamy luu :
🥰
2026-10-15 08:20:06
0
To see more videos from user @imadiabeid, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About