@bongofive: Burkina Faso inapanga kurejesha mashindano ya Miss kwa mfumo mpya utakaoweka mkazo katika utamaduni wa Kiafrika, mavazi ya heshima, mitindo ya nywele za asili na uwezo wa akili wa washiriki. Waziri wa Utamaduni, Pingdwendé Gilbert Ouédraogo, amesema mashindano hayo yanapaswa kumthamini mwanamke wa Burkina Faso zaidi ya urembo wa mwili pekee. Je, huu ni mwelekeo ambao nchi nyingine za Afrika zinapaswa kuuangalia? @cathed__