@jambotv_: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Wakili Msomi Boniface Mwabukusi amehojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo Baraza la Uongozi la TLS kupokea fedha za 'kufadhili' maandamano ya Oktoba 29, 2026. Hayo yameelezwa na Wakili wa Mwabukusi Jebra Kambole leo Oktoba 15, 2026 mara baada ya mteja wao kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana. "Hakuhojiwa kama mtuhumiwa amehojiwa kwa kifungu cha 36(2)(c) cha Sheria ya Ushahidi kwa hiyo amehojiwa kama shahidi...amehojiwa kwa tuhuma kwamba TLS imeacha kufanya shughuli zake kama Rais wa TLS anafanya shughuli za kiharakati akajibu kuwa TLS inafanya shughuli za kiharakati za kitaaluma" Kwa mujibu wa Jebra mteja wao alionyeshwa video mbalimbali zenye matamko yake ikiwemo aliyowahi kuyatoa wakati wa sakata la bandari la DP World pamoja na hotuba zake alizozitoa kwa miaka kadhaa. "Kulikuwa na tuhuma kwamba Baraza la Uongozi la TLS lilipokea fedha kwa ajili ya kufadhili maandamano ya tarehe 29 Oktoba mwaka 2026 ambayo hayajatokea alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo alizikana tuhuma hizo kwamba baraza la uongozi halijawahi kukaa juu ya maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2026" Baada ya mahojiano Mwabukusi alidhaminiwa na Jebra Kambole pamoja na Ziada Mkwazu kwa masharti kuwa muda wowote atakaoitwa na ZCO atatakiwa kwenda.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 15 October 2026 16:10:39 GMT
21022
697
26
25

Music

Download

Comments

baba123mimi
Baba mimi :
hii serikali inaelekea kuchanganyikiwa
2026-10-15 17:49:57
4
user4107610819756
[email protected] :
nyny mnareta taaruki ebu fateni utaratibu washeria mtutetee sio kuwa mwanaharakat
2026-10-15 19:55:27
0
lipangala
Lipangala :
Kwenye DP world mwambukusi alitudanganya sana.TLS imebaki kua Wana harakati tu hakuna ueledi tena
2026-10-15 17:45:07
0
user8249134183606
user8249134183606 :
wasomi wanaongea
2026-10-16 11:54:14
0
ramadhani.amir2
Ramadhani Amir :
ila Tanzania hapana
2026-10-16 14:20:54
0
mbayanisinyock
Mbayani Sinyock :
ata simwelew aise
2026-10-16 07:21:09
0
k.rang7
k rang :
mchochez aliacha siasa hv nyinyi hamkuona akiyafanya hayo lini alikemea mchochez huyo alisaport hayo
2026-10-16 08:00:59
0
brotherhasao
HASAO :
video ninayotumia nguvu kubwa kusikiliza sinaga mda , kama mmeshindwa kuweka sauti kubwa futeni
2026-10-16 06:04:12
0
user7870265676119
selesti :
mmmmmm mungu yupo bize sana
2026-10-15 18:58:25
0
king.david2702
King David :
hahaha
2026-10-15 17:38:17
0
kombe5930
kombe :
Duu sasa mbona nishida
2026-10-15 17:37:42
0
kasuguguboy
KASUGUGU :
kumbe Kuna maandamano Oct 2o??
2026-10-15 19:40:32
0
nhamalangosha
Nhamala Ngosha :
Kuna vitu vinatia hasira sana ... Mungu ni mwema sana endelea usiache kutimiza majukumu yako
2026-10-15 17:28:20
0
user7463278123571
user7463278123571 :
Ile tume ya lila itakuja na majibu yote
2026-10-15 17:02:40
0
rajabu.shekland
Rajabu Shekland :
Samia anahangaika xana kuficha mauwaji ila kwa mungu haina kificho
2026-10-15 16:40:27
0
imma.furniture
imma furniture :
mbona dumbia anapiga pembeni tu kila mara
2026-10-16 05:49:18
0
bronijofresalele
Broni jofre Salele :
wqmesha anza kutaka kuwabambikia watu kesi kama mange alivo sema kwenye hiyo tume halam, ya lila
2026-10-16 10:58:11
0
manjalesitta67gma
[email protected] :
🥰🥰🥰
2026-10-15 16:51:50
0
user4839868190750
kim :
🏅🏅🏅
2026-10-15 19:12:50
0
olemanduk6
olemanduk :
🥰🥰🥰
2026-10-15 17:05:21
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About