@uhondo.tv: Ngome ya Fort Ikoma iliyopo katika eneo la Ikoma, pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti, ni miongoni mwa maeneo yenye historia ya utawala wa kikoloni nchini Tanzania, ambayo sasa inaendelea kuwa kivutio cha utalii wa historia na michezo kupitia uwanja wa gofu uliojengwa katika eneo hilo. Ngome hiyo ilijengwa wakati wa ukoloni wa Wajerumani kwa ajili ya uangalizi na udhibiti wa shughuli katika eneo hilo, ikiwemo kufuatilia maliasili na wanyamapori waliopatikana kwa wingi. Eneo la juu la Ikoma lilichaguliwa kutokana na uwezo wake wa kutoa mwonekano mpana wa maeneo yanayolizunguka, huku historia yake pia ikihusishwa na mapambano ya jamii ya Ikoma dhidi ya utawala wa kikoloni. Baada ya matumizi ya kikoloni, eneo hilo lilitumika pia kwa mafunzo ya maofisa wa Jeshi la Tanzania kabla ya kukabidhiwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kusimamiwa na Hifadhi ya Taifa Serengeti. Kwa sasa, Fort Ikoma inaunganisha urithi wa kihistoria na utalii wa kisasa, ambapo wageni wanapata fursa ya kujifunza historia ya eneo hilo, kutembelea Serengeti na kushiriki mchezo wa gofu, hatua inayopanua wigo wa vivutio vya utalii nchini Hususani katika hifadhi ya Serengeti #serengeti_national_park #UhondoTVUPDATES
Uhondo TV
Region: TZ
Thursday 15 October 2026 16:15:06 GMT
Music
Download
Comments
George Omary :
🥰🥰🥰
2026-10-15 16:33:26
0
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm
homepage.