@jamiivoice_: HABARI: Aliyekuwa mgombea urais kupitia ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, ametoa wito wa kusitishwa kwa makongamano yanayojadili hali ya kisiasa nchini kwa sasa, akidai kuwa yanapoteza muda na huenda yakatumika kuuhadaa ulimwengu kuwa Watanzania wameweza kutatua mgogoro wa kisiasa bila msaada wa nje. Mpina amesema badala ya kuendelea na makongamano hayo, Watanzania wanapaswa kuunganisha sauti zao na kuiomba jumuiya ya Afrika na ya kimataifa kuleta msuluhishi huru atakayezipa pande zinazohasimiana nafasi ya kusikilizwa na kutafuta suluhisho la mkwamo wa kisiasa nchini. Ametaja wananchi, wanasiasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini, vyombo vya habari na makundi mbalimbali ya kijamii kuwa miongoni mwa wadau wanaopaswa kushiriki katika wito huo, akisisitiza umuhimu wa kupata jukwaa litakalowezesha pande zote kueleza malalamiko yao. Akizungumza na wanahabari, Mpina amesema mjadala wa mgogoro wa kisiasa haupaswi kupuuza madhara ambayo amedai yamewapata Watanzania, akitaja vifo, watu waliojeruhiwa na kupata ulemavu wa kudumu pamoja na wengine ambao hawajulikani walipo. Katika maelezo yake, Mpina ametaja majina ya Balozi Humphrey Polepole, Deus Soka, Mdude Nyagali, Dioniz Kipanya na Shadrack Chaula miongoni mwa watu ambao amesema hawajulikani walipo. Hata hivyo, hali ya kila mmoja na mazingira ya kutoweka kwao yanahitaji kuthibitishwa kwa taarifa huru. Aidha, Mpina amedai kuwa baadhi ya wapinzani, akiwemo Tundu Lissu, David Levi Nkindikwa maarufu Kijana Mzalendo na Jackson Myawami, wako magerezani kutokana na kesi alizozitaja kuwa za kisiasa. Pia amekosoa mwenendo wa uchaguzi na namna kesi za wagombea zilivyoshughulikiwa mahakamani. Mpina ameitaka jamii kuendelea kupaza sauti kuhusu masuala hayo, akisisitiza kuwa suluhisho la mgogoro wa kisiasa linapaswa kuhusisha pande zote zinazohasimiana na kuzingatia malalamiko yao.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 16 October 2026 05:14:33 GMT
35623
579
4
8

Music

Download

Comments

user1086509016597
[email protected] :
Asante kwa kutkmbusha tunaendelea kuwaombea mungu yupo upande wao
2026-10-16 06:41:25
1
ki.utu
Kabuki :
Kweri
2026-10-16 08:33:10
0
ummy.salehe79
mom firadaus 💞💞 :
iko siku mungu atashusha mkono wake juu yao🥲🥲
2026-10-16 07:50:03
0
zogo.babalao
Zogo Babalao :
Usitende Uhalifu kwa kutegemea Jina lako....!!
2026-10-16 15:00:20
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About