@cawabemedia_: Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amemuondoa katika nafasi yake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Songwe, Mhandisi Fredrick Mande, na kumtaka kurejea makao makuu ya taasisi hiyo. Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kile kilichoelezwa kuwa kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa ujenzi wa barabara ya Forodha–OSBP Tunduma, yenye urefu wa mita 1,675 katika mpaka wa Tanzania na Zambia. Kadogosa amesema hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa ili kumpata meneja mwingine atakayesimamia shughuli za TANROADS katika Mkoa wa Songwe. Uamuzi huo umefuatia ziara ya Waziri Kadogosa ya kukagua maendeleo ya mradi huo usiku wa Oktoba 15, 2026, akitekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi. Awali, Ndejembi alieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo, licha ya Serikali kuwa tayari imelipa sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wake. Mradi huo unalenga kuboresha mtiririko wa magari na kupunguza msongamano wa malori katika Kituo cha Forodha cha Tunduma, ambacho ni kiungo muhimu cha biashara kati ya Tanzania na Zambia.

cawabemedia
cawabemedia
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 16 October 2026 06:05:38 GMT
18379
420
15
18

Music

Download

Comments

ranadhanirajabu
R50 :
Safi maana upande wa Zambia foleni mpk dereva mmoja kampuni ya MA amefariki kwenye foleni
2026-10-16 08:42:55
0
mtu.pori59
Mtu pori :
kazi zakupeana ndio tatizo
2026-10-16 17:17:49
0
saidimwakibe
Copper 2 :
Barabara nyingi za TANZANIA zinashimo hatari ata atujui shida nini
2026-10-16 14:25:37
0
mbilinyi634
Mbilinyi :
Point ziliwapumzisha kujenga barabara
2026-10-16 22:00:25
0
jumanne.ally959gm
Jumanne [email protected] :
warudishe pesa hawo
2026-10-16 06:23:01
0
agnesimwanyika6
bg bos :
Ndio cement ni tatizo mwacheni
2026-10-16 11:09:12
0
user283844804321
simba :
ndio matatizo walandarasi wazawa
2026-10-16 08:19:04
1
wilfredpaul
[email protected] :
njoon kahama ndio utajua nini kinaendelea
2026-10-16 13:42:38
0
khatib.mrisho
Khatib Mrisho :
😳😳😳
2026-10-16 19:12:35
0
chrispinmwampina
heis_pino :
🥰🥰🥰
2026-10-16 18:55:24
0
danielboniphace6
I don't care ⛎ :
😁😁😁
2026-10-17 05:20:17
0
jumanne.ally959gm
Jumanne [email protected] :
💯💯💯
2026-10-16 06:21:55
1
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About