@dhahabuonlinetv: KADOGOSA AMWONDOA MENEJA WA TANROADS SONGWE KATIKA NAFASI YAKE. Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amemuondoa katika nafasi yake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Songwe Mhandisi Fredrick Mande, na kumtaka kurejea makao makuu ya TANROADS, kufuatia kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa ujenzi wa barabara ya Forodha - OSBP - Tunduma yenye urefu wa mita 1,675, mpakani mwa Tanzania na Zambia. Amesema hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa ili kumpata meneja mwingine atakayesimamia shughuli za TANROADS katika Mkoa wa Songwe. Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Kadogosa kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo usiku wa Oktoba 15, 2026, akitekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ambaye awali alieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo licha ya Serikali kutoa sehemu kubwa ya fedha za mradi. Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuboresha mtiririko wa magari na mizigo katika mpaka wa Tanzania na Zambia, Kupunguza msongamano wa magari, kuongeza ufanisi wa huduma za forodha na kurahisisha huduma za biashara za kikanda umeoneshwa kusuasua licha ya kutakiwa kukamilika ifikapo Oktoba 31, 2026 kwa mujibu wa kimkataba. Aidha, Kadogosa amempa mkandarasi wa mradi huo muda wa wiki mbili kukamilisha kazi zilizobaki, huku akiahidi kurejea eneo hilo ndani ya siku saba kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa na kujiridhisha kuwa kasi ya ujenzi imeongezeka. Kadhalika, Waziri huyo ametoa maelekezo kwa Mameneja wote wa TANROADS nchini kuhakikisha kila mradi wa ujenzi unasimamiwa kwa uwazi na uwajibikaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa pande tatu zenye majukumu tofauti, ambazo ni msimamizi wa mradi, mkandarasi na msimamizi anayewakilisha Serikali. Waziri Kadogosa, ameonya dhidi ya hali ya wasimamizi wa miradi kuegemea maslahi ya upande mmoja, akisema mwenendo huo unaweza kudhoofisha usimamizi huru na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya Serikali. Awali Makamu wa Rais Mhe. Deogratius Ndejembi katika ziara yake, alisisitiza kuwa Serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi ya miundombinu kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, hivyo ni wajibu wa watendaji na wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa fedha ili wananchi wanufaike, hivyo tunatakiwa kusimamia kazi ili fedha hizo ziongeze thamani na manufaa kwa wananchi,” alisema Ndejembi. Alieleza kuwa taarifa alizopokea zilionyesha kuwa mkandarasi alikuwa amelipwa Shilingi bilioni 4.4 kati ya Shilingi bilioni 6.8 za mkataba, sawa na zaidi ya asilimia 60 ya thamani ya mkataba. Hata hivyo, maendeleo ya ujenzi hayakuendana na kiwango cha malipo yaliyokuwa yamefanyika.

DHAHABU ONLINE TV
DHAHABU ONLINE TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 16 October 2026 06:22:36 GMT
28973
1075
27
45

Music

Download

Comments

abdullahqassim1
BEACH BOY :
hayo maigizo tuu
2026-10-16 16:39:42
3
trasport450
Trasport :
nipo sankanya kwoo mnataka kunindanganya mpaka nafka tunduma itakuwa tayali ety
2026-10-16 21:04:28
0
lyon270
GUNPLAY :
Hao ni matapeli banaa yani icho kipande cha kilometer 1 na nusu wanajenga sasaivi ni mwaka unaisha wamesababisha foleni ya kuvusha magari imekua kubwa mnoo wazambia wenzetu washamaliza kipande chao tumebaki kwetu ni aibu sanaa aisee
2026-10-16 19:43:00
1
harry.jackson085
Harry Jackson :
Jamani bos wangu wa kampun ya narma nini tena jaman pole sana
2026-10-16 10:44:20
0
oscarhananda
Oscar Hananda :
kiukweri viongozi tulikuwa nao zamani Mungu akawapenda leo tumawababaishaji2
2026-10-16 19:40:42
0
josephmawala
Joseph Robinson :
tatizo 10%
2026-10-16 17:00:36
0
stevedossa15
Steve Dossa :
hiyo Tunduma mpaka mbeya ni tatizo saaana
2026-10-16 12:51:31
0
mjiga19
mjiga :
safi sanaa huyu Anatufaa sana
2026-10-16 14:24:33
0
mr.mol7
Mr mol :
NANI NI NANI
2026-10-16 10:33:24
0
gilelugala
4G :
cement inasumbua hata huku njombe
2026-10-16 13:14:43
0
maishanivita
mwakimtha mbilinyiamigo329@gma :
hawa walio shika tarumbeta alikuwpo nae
2026-10-16 15:42:31
0
obadia04
obadialasima :
sementi imepanda bei
2026-10-16 08:44:24
0
utukufu.na.haki
utukufu na haki 🔥🔥🔥 :
kwakweli tunduma ishu ya barabara ni kero sana
2026-10-16 14:09:41
0
user6224029813106
neema mwasomola :
Tena wameona umekuja mbeya ndio wanafanya kazi ngoja undone wanaacha
2026-10-16 10:48:23
0
danielfrank7085
Daniel Frank :
sanaa
2026-10-16 10:41:53
0
abby_dart_boe
Mr Ability. 🧔 :
bora maana tunduma ulaji mlizidi nyie mameneja
2026-10-16 11:25:09
0
stevedossa15
Steve Dossa :
mzee Kadogosa hao Wana mwaka mmoja umeisha hakuna kitu,sio miezi 3
2026-10-16 12:52:25
0
harry.jackson085
Harry Jackson :
Achen kumnyanya bos wangu wa zamani narmo, barabara ya mbeya kuanzia nsalaga hadi mbaliz ifis inamiaka mingapi toka iyanze, tunakula vumb tuu, hafu mnatuambia tusiteme mate
2026-10-16 10:53:19
0
abdul.makwizi
Abdul Makwizi :
aoni matapeli ao wezi tuu wajenzi wa uyo barabara ichokipande kitajengwa miaka mi 5 icho kipande chenyewe ni kilometa 4 tuu kitatengenezwa miaka kibao apo
2026-10-16 21:55:20
0
hamisitenekumwiku
teneku 444 :
ww waziri husika ulikuwa wapi mpk makamu wa rais kaja na ww ndo unaibuka mzee,,
2026-10-16 15:58:35
0
mr.mp26
MP.26 :
Lami zenyewe zinaviwango?
2026-10-16 15:09:27
0
cosmasantony3
cosmasantony123 :
sehemu yenyewe hata km 10 haifiki inamalinza mwaka shinda nin pesa hamuna au usimamizi mbovu
2026-10-16 16:36:08
0
stevedossa15
Steve Dossa :
kiongozi.kuwa muongo ni shiida saaana
2026-10-16 12:50:14
0
redscorpion355tz
@RED SCORPION 🦂 🇹🇿🇺🇬🇰🇪 :
ngoo moshibaa tu bombambili Hadi kwamuhaya yaani mh utajiuliza hii ni dar es salaam ilala au, maana Hadi mabasi asilimia kubwa yanaogopa kwenda Sasa mvua inyeshe ndio kabisa watu makazini hawaendi usafiri hakuna
2026-10-16 11:18:34
0
michael.zacharia1
Michael Zacharia :
njoo na iringa balabala ya igumbilo
2026-10-16 10:24:28
0
To see more videos from user @dhahabuonlinetv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About