@millardayo_: Kampuni ya kutengeneza magari yanayotumia umeme ya Tesla, inayomilikiwa na Bilionea Elon Musk, imetambulisha gari jipya aina ya Tesla Roadster lenye uwezo wa kunyanyuka kutoka ardhini na kufanya sarakasi angani kwa kutumia teknolojia iliyotengenezwa kwa ushirikiano na kampuni ya SpaceX. Gari hilo limetambulishwa Oktoba 15, 2026, katika kituo cha majaribio ya roketi cha SpaceX kilichopo McGregor, Texas Nchini Marekani, ambapo limeonesha uwezo wa kupaa kwa muda mfupi, kujigeuza angani na kutua ardhini kwa usalama. Katika majaribio hayo, gari hilo limeonesha uwezo wa kuruka juu ya magari mengine matano ya Tesla, huku likitumia mfumo maalumu wa hewa iliyoshinikizwa kwa nguvu ili kujiinua kutoka ardhini. Aidha, Tesla imesema gari hilo lina uwezo wa kuongeza kasi kutoka sifuri hadi takribani kilomita 100 kwa saa ndani ya sekunde moja, huku Elon Musk akieleza kuwa Kampuni hiyo inalenga kuanza uzalishaji wake mwaka 2028. #MillardAyoUPDATES
millardayo
Region: TZ
Friday 16 October 2026 07:40:59 GMT
Music
Download
Comments
Vaileth Kessy 🦋🦋 :
nitafute hela sasa ili nikwepe foleni😊😊😊😊
2026-10-16 07:44:01
532
just me ✨️✨️✨️ :
ndo naenda kutoa Figo hvyo 😁
2026-10-16 08:39:23
286
~lucy~💖💞 :
Hii itanifaa kwenye foleni😂😂😂
2026-10-16 07:44:28
357
Sunset :
Musk will change the world forever and siku tunashtuka tushachelewa
2026-10-16 08:31:06
10
thattvenny❤️ :
Mpk tuuze roho safari hii😂💔
2026-10-16 07:45:14
58
H.U.N.C.H.O :
mkuu atupumzishe sasa wajameni
2026-10-16 07:45:56
61
Heaven💞Gel💕 :
Elon musk aya matus sas😅
2026-10-16 11:31:44
1
Fine girl🦋🧚♀️ :
Sasa tulipaa wote barabarani Nani atakaa kwenye foleni 😂😂😂😂
2026-10-16 09:41:17
45
Mrs wakutrend :
yasifike Tanzania haya mbona ndege zitakosa njia hangani mana folwn kidogo mtu anataka apae😂😂
2026-10-16 07:44:36
61
Swaum Ally :
ikifika tanzania itapaa muikute ikulu imegonga suluuu 😁
2026-10-16 10:11:46
83
Abdoulkadrihudi17🇧🇮 :
no one can steal my sticker
2026-10-16 12:14:36
7
s :
uliza bei alafu anitumie ww utakuwa dalali [Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-16 10:10:50
1
Dhel Belle :
jina la movie pls
2026-10-16 17:23:08
1
fedhasongoro :
Kwan musk ni nani🤣
2026-10-16 08:01:45
20
Otto🪖 :
millard
2026-10-16 12:36:04
0
bestie :
zikitoka copy nishituen [Big LOL]
2026-10-16 08:15:35
2
pale kinegembasi :
kwel
2026-10-16 07:46:04
25
🫧Zane🧸 :
Imeruka ama imepaa!?
2026-10-16 08:05:18
7
Themadboy87 :
mmh mmh nilotaga hii ndot 2016 kumbe hilikuwa ya kweli bwana...mungu sio kiziwii anasikia kila maombi ya mtu😏😏
2026-10-16 12:55:11
5
Gift 💕🦋 :
Bilioni ngap 😅😅😅
2026-10-16 07:45:25
20
vash_shine🦋♓️ :
Overtaking zitakua zakibabe sana😅 utaskia kwe taarifa magari yagongana angani😂😂
2026-10-16 09:29:10
26
Rakheem :
hii tunafundishwa VETA kuiendesha au...😂😂
2026-10-16 12:20:52
16
Anier Ameer :
mbona ina geuka geuka sintatapika😳.
2026-10-16 11:41:33
6
happy pesambili :
atapanda yeye na familia yake 😂😂😂
2026-10-16 07:43:29
8
twenty one :
SAWA GARI LINAPIGA SARAKASI ANGANI, LAKN SIJAELEWA LENGO LA GARI KAMA HIO NINI ??? MAANA HAYA YASIOPAA TU AJALI ZIMETOSHA
2026-10-16 11:39:37
5
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm
homepage.