@millardayo_: Mahakama Kuu ya Tanzania imeuagiza Uongozi wa Gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam kuhakikisha Mawakili na Washauri wa kisheria wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu wanaruhusiwa kukutana na kuzungumza naye kwa usiri bila mazungumzo yao kusikilizwa na Maafisa wa Magereza. Kwa mujibu wa taarifa ya uamuzi huo uliotolewa leo, Oktoba 16, 2026, katika Shauri Na. 7300/2026 lililofunguliwa na Wakili Kulwa Maduhu na wenzake, Mahakama imeeleza kuwa Maafisa wa Magereza wanapaswa kusimamia usalama kwa kukaa umbali unaowawezesha kuona mazungumzo yanapofanyika, lakini si kusikia kinachozungumzwa. Akisoma uamuzi huo, Jaji Amir Mruma, aliyeongoza Jopo la Majaji watatu, amesema Maafisa wa Magereza wanapaswa kuzingatia Kanuni ya 13 ya Kanuni za Uendeshaji wa Magereza za mwaka 1968, inayotaka mashauriano kati ya Mfungwa na Wakili au Mshauri wake wa kisheria yafanyike kwa usiri. Aidha, Mahakama imeeleza kuwa kuzuiwa kwa Wakili Maduhu kuingia Gereza la Ukonga Oktoba 28, 2025, kwa sababu jina lake halikuwapo kwenye orodha ya Mawakili iliyowasilishwa na Lissu, hakukuwa na sababu ya kutosha ya kumnyima fursa ya kuonana na mteja wake. Mahakama pia imewaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Jenerali wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga kuhakikisha Mawakili wa Lissu wanapofika gerezani wanapata fursa ya kufanya mazungumzo na mashauriano na Mteja wao bila kuingiliwa wala kusikilizwa. #MillardAyoUPDATES

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 16 October 2026 11:03:41 GMT
19884
786
20
11

Music

Download

Comments

morgan_msuya
MSUYA❦ :
Natafuta mdada mwenye mimba twende clinic ili nipate net, mbu wataniua jamani 🥲
2026-10-16 11:49:43
3
toniton2533
A Thousand :
hii taarifa ya lini
2026-10-16 11:11:22
2
user4278778553851
mtanga zoka kulu :
𝘴𝘪𝘸𝘢𝘮𝘦𝘴𝘦𝘮𝘢 𝘩𝘶𝘬𝘶𝘮 𝘪𝘯𝘨𝘦𝘵𝘢𝘬𝘪𝘸𝘢 𝘪𝘵𝘰𝘬𝘦 𝘵𝘳𝘩 6 𝘪𝘮𝘦𝘬𝘶𝘢𝘫𝘦 𝘮𝘱𝘢𝘬𝘢 𝘭𝘦𝘰
2026-10-16 12:46:15
0
barakakayungilo37
baraka kayungilo.tz✅✅ :
et
2026-10-16 11:19:17
1
moudyrasta1
💌Moud✍️ R@$T@🌎 :
父親
2026-10-16 11:11:26
1
qis59916
qis :
kesi imeisha uamuzi huo utasaidia nini?labda kesi zijazo
2026-10-16 13:47:50
0
sir.ngure5
Sir ng'ure :
Mungu endelea kutenda miujiza amen
2026-10-16 15:14:57
0
mumyb248
Firstborn wao💫❤️🤗 :
Sawa sawa
2026-10-16 13:39:07
0
israeliyohana379g
[email protected] :
hii ccm inahangaika sana
2026-10-16 14:01:06
0
user2858613612375
user2858613612375 :
2026-10-16 12:48:26
0
merry.riziki
Merry Riziki :
wanaaza kukubali.
2026-10-16 12:19:56
1
nabwangi
CHIEF :
Ngoja nimalize kula niseme kachochote
2026-10-16 11:29:22
1
sandesteven769
Sande Steven :
mambo yatanyooka tu huyu lisu tutampambania hatakama watapindisha sheria
2026-10-16 14:36:00
0
deo.mwalise
Deo Mwalise :
✌✌
2026-10-16 13:43:08
0
micajunia
micajunia :
🙏
2026-10-16 12:46:45
0
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About