@rocky.is.my.name: Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, ameibua vicheko baada ya kutoa kauli inayowalenga waliopost wimbo wa Libasse Moto, unaohusishwa na mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye. 🎙️ Akizungumza katika Uwanja wa Azam Complex, Kamwe amesema kwa utani kuwa wale waliopost wimbo huo hawatapewa vitambulisho (ID) vya kuingia kwenye mchezo wa Yanga wa kesho. 😂 “Kama ulipost nyimbo ya Libasse Moto, kesho hupati ID!” Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya Simba SC kuifunga Yanga mabao 2-1 kwenye Kariakoo Derby iliyochezwa Oktoba 10, 2026. 🔥 Wakati mashabiki wa Simba wakiendelea kufurahia ushindi wa dabi, Yanga inaelekeza nguvu kwenye mchezo wake wa CAF Champions League dhidi ya CFFA ya Madagascar, utakaochezwa Jumamosi, Oktoba 17, katika Uwanja wa Azam Complex. Kauli ya Kamwe kuhusu ID imeongeza ladha ya utani wa kisoka kati ya watani wa jadi, huku wimbo wa Libasse Moto ukiendelea kuwa sehemu ya mijadala ya mashabiki. 🤣 SWALI KWA MASHABIKI: Hivi wale waliopost wimbo wa Libasse Moto wafanye nini sasa ili Ally Kamwe awaruhusu kuingia uwanjani? 😂 ⚽ ROCKY SPORTS | EVERY MATCH MATTERS. #RockySports #AllyKamwe #YangaSC #SimbaSC #libassegueye
ELNINO 🌧️ — MVUA YA MIKEKA
Region: TZ
Friday 16 October 2026 18:28:56 GMT
Music
Download
Comments
BLACK SHADOW :
😂😂😂😂😂😂😂 libase motoooooo libase fire💪💪💪💪💪💪💪💪
2026-10-17 07:15:42
1
Ibrahimu Kaven :
kaweka
2026-10-17 00:34:00
1
geofreymwafinga :
🤣🤣🤣🤣🤣 ila aly kamwe hajuag kuchukia yn amejaa utan mwingi kaka yupo poa sn nmependa
2026-10-17 05:11:12
1
bahatboy :
🥰🥰🥰
2026-10-16 20:04:23
1
To see more videos from user @rocky.is.my.name, please go to the Tikwm
homepage.