@tumaini_pr_tv: Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamsaka Peter Kiariro, Mkazi wa Maore, Wilaya ya Same kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Bernard Kiluwa (26), Mkazi wa Kijiji cha Mheza, Kata ya Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 16, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, tukio hilo limetokea usiku wa Oktoba 12, 2026, katika Kitongoji cha Kalemane, Kijiji cha Mheza, Kata ya Maore, Tarafa ya Naungu, Wilaya ya Same. Uchunguzi wa awali wa Polisi umebainisha kuwa chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa wivu wa kimapenzi, baada ya Marehemu kucheza muziki kwa muda mrefu na Mke wa Mtuhumiwa wakati wa sherehe ya ubarikio iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwa Shabani Rajab. Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa alimwomba Marehemu waende pembeni kwa ajili ya mazungumzo, lakini baadaye alimshambulia kwa kutumia kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa kisu na kumjeruhi tumboni na kifuani kabla ya kutoroka eneo la tukio. #tumainiprtv #tboyliontz #hapaninyumbanikwawote
Tumaini pr Tv
Region: CA
Friday 16 October 2026 19:54:56 GMT
Music
Download
Comments
Ester Mwaki💞 :
Hatar sana
2026-10-17 08:37:45
0
To see more videos from user @tumaini_pr_tv, please go to the Tikwm
homepage.