@nyebowsa_media: Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, maarufu kama Simba, ameendelea kuiwakilisha Tanzania kimataifa baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya Top African Celebrity of the Year 2026 katika tuzo za Africa Golden Awards 2026. Tuzo hiyo inamtambua Diamond kama mmoja wa watu mashuhuri barani Afrika, kutokana na umaarufu wake na mchango wake katika tasnia ya burudani. Ushindi huo ni heshima kwa Diamond Platnumz na Tanzania kwa ujumla, huku ukiendelea kuonesha nafasi na ushawishi wa wasanii wa Kitanzania katika tasnia ya burudani barani Afrika. #nyebowsamedia #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #diamondplatnumz #eastafrica