@gillybonny_tv: Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Pwani, Samaha Seif Said, amekemea vikali kauli ya Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akidai kuwa imewadhalilisha na kuwakatisha tamaa vijana wanaojitolea kukitumikia chama hicho. Samaha amesema kauli ya Mchengerwa, aliyesema vijana hawafanyi kazi bila kupewa hongo na kwamba wamechagua upande, si njema kwa vijana wa UVCCM, huku akieleza kuwa wako tayari hata kuomba Radhi endapo itabainika wamemkosea lakini Kwa makubaliano ya Kistaarabu na Maslahi ya Umoja kuliko kuziachia kauli zake kama ambavyo amefanya . Akizungumza kuhusu kauli hiyo iliyotolewa na Mchengerwa mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Pwani, Samaha amesema kauli hiyo imewaumiza vijana na kuhoji sababu za kuwahusisha na rushwa wakati si kipindi cha uchaguzi. “Kauli hii imeniuma na si njema kwa vijana. Kama kuna sehemu tumekosea, Mchengerwa ana nafasi ya kutuita na kutueleza, nasi tuko tayari kumuomba radhi kama tumemkosea. Lakini kwa nini anasema vijana wamechagua upande na kuwaita wala rushwa? Je, ni kweli hatufanyi kazi bila rushwa?” amehoji Samaha. Aidha, Samaha amemtaka Mchengerwa kutaja wazi mtu au watu anaowalenga ikiwa ana malalamiko binafsi, badala ya kutumia kauli zinazoweza kuchafua taswira ya jumuiya nzima, akisisitiza kuwa vijana wa UVCCM wanajitolea kwa ajili ya chama na hawapaswi kudharauliwa.

Gilly Bonny Tv
Gilly Bonny Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 17 October 2026 15:30:50 GMT
3941
78
1
14

Music

Download

Comments

katabazi_star
Katabazi Starpinus :
[Pray]
2026-10-17 19:21:56
0
To see more videos from user @gillybonny_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About