@mn_boxing_media_tanzania: Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Pius Saimon Mpenda, maarufu kama Mpenda 9Jr, usiku wa kuamkia leo nchini United Arab Emirates (UAE), amedhulumiwa matokeo ya pambano lake la kimataifa. Mpenda alicheza pambano la raundi nane dhidi ya bondia Qasim Abudabaat, raia wa Jordan, ambaye alikuwa hajawahi kupoteza. Pambano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Emirates Sports Hotel jijini Dubai nchini UAE na kuishia kwa matokeo ya sare. Jaji namba moja alimpa Mpenda ushindi wa pointi 77–75, huku jaji namba mbili akimpa Abudabaat ushindi wa pointi 77–75, na jaji wa mwisho akitoa sare ya pointi 77–77. Matokeo ambayo hayakuwa halali kwa bondia Mpenda, ambaye alionyesha mchezo mzuri na kutawala pambano hilo katika raundi nyingi zaidi ya mpinzani wake huyo. Na endapo Mpenda angeshinda pambano hilo, basi angeandika historia nyingine kwa upande wake ya kushinda pambano lingine la kimataifa nchini humo. Itakumbukwa kuwa Mei 20, 2023, aliwahi kumpiga bondia Moughti El Moutaouakil, raia wa Morocco, kwa matokeo ya 'TKO' kwenye raundi ya nane kati ya raundi nane. Mpenda anazidi kuwa bondia hatari na mwiba mchungu pindi anapokwenda kucheza mapambano ya kimataifa nje ya mipaka ya Tanzania, huku akitoa nkong'oto kwa wapinzani wake na kudhulumiwa matokeo. Itakumbukwa kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Novemba 22, 2025, nchini Saudi Arabia, Mpenda alicheza pambano la raundi sita dhidi ya bondia Julius Porras Ruiz, raia wa Mexico, ambaye alikuwa hajawahi kupoteza, na matokeo ya pambano hilo yakawa sare. Aprili 25, 2025, nchini Urusi, Mpenda alicheza pambano la raundi sita dhidi ya bondia Vyacheslav Nazarov, raia wa Urusi, na matokeo ya pambano hilo pia yakawa sare. Mpaka sasa, katika maisha yake ya ngumi, Mpenda amecheza jumla ya mapambano 10 ya kimataifa nje ya mipaka ya Tanzania, ambapo ameshinda mapambano matatu, amepoteza manne na kutoka sare mara tatu akitwaa mikanda miwili WBU nchini Uganda na WBC Peace nchini Uturuki. Hili ni jitu la Mtumba, Pius Mpenda!. Sema zile Uppercutt za Katavi Boy, Mjordani supu atakunywa mchuzi tu nyama atazifaidi mwakani (Utani) 😁. Mn Boxing Media Tanzania #boxing #michezo #azamtv #tanzaniaboxing #wasafifm
Mn Boxing Media Tanzania
Region: TZ
Saturday 17 October 2026 15:58:25 GMT
Music
Download
Comments
Official dostar🎙️ :
mpenda wa moto
2026-10-17 20:16:32
0
Khadege :
tumeonewa apo duh mzungu tumembonda
2026-10-17 19:37:08
0
Chris Nize :
awo sasa ndo wana uchungu na hii nchi hongera bro
2026-10-17 19:44:59
0
mubbah :
Mtu wa kazi ngumu
2026-10-17 21:05:41
0
Leonard Msoya :
👍👍👍🫡🫡
2026-10-17 17:35:43
0
To see more videos from user @mn_boxing_media_tanzania, please go to the Tikwm
homepage.